DODOMA
Wakulima wa manispaa ya Dodoma
wameiomba serikali kuboresha mfumo wa uendeshaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi
Wakizungumza na Dodoma fm
wakulima wa mkoa wa Dodoma wamesema hawanufaiki chochote tangu kuanzishwa kwa mchakato huo wa sense ya watu na makazi.
Nae bw. Mafita maulid ameiomba serikali kuboresha
huduma mbalimbali za jamii iliwaweze kujua umuhimu wa sense.
Akizungumzia swala hilo mchambuzi wa masuala ya sensa Bw Kenedy Nteminyanda amesema
ni vema sense ya watu na makazi ingesaidia katika kumaliza swala na
migogoro ya wakulima na wafugaji.
Wakazi wa manispaa ya Dodoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya
kuadhimisha siku ya damu duniani itakayo fanyika tarehe 14 Juni mwaka huu.
Wakizungumza na kituo
hiki bi.Frora kamwela ambaye ni muuguzi
na mshauri nasaha wa kitengo cha damu salama amesema maadhimisho ya siku ya damu Duniani kwa mkoa
wa Dodoma yatafanyika katika kituo chao kidogo cha Benki ya Damu.
Aidha Bi. Frola amesema a
anawaomba watu wawe na umoja katika suala la kuchangia damu kwani suala la kuchangia damu salama ni jukumu letu
sote.
Pia amesema kuwa endapo utajitokeza katika suala zima la kujitolea damu salama
utapata kadi na itakusaidia popote uendako nchini kama utakuwa na tatizo la
kutaka damu utapewa bila gharama yeyote.
Sanjari na hayo Bi.Frola kamwela amesema kila mmoja
anaruhusiwa kutoa damu isipo kuwa mtu mwenye
tatizo la sukari,presha ya kupanda au ya kushuka,pamoja na magonjwa
mengine.
Serikali
kupitia wizara ya ardhi nyumba maendeleo na makazi imekiri kuwepo na matatizo
ya ardhi isiyopimwa nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi nyumba
maendeleo na makazi Prof. Anna Tibaijuka
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Bi Muhonga Luhanywa
lililohoji kwa nini serikali isiwe na mpango wa kupima ardhi ili kuondoa
ujengaji holela mijini na vijijini
Aidha Prof. Tibaijuka ametanabaisha kuwa
kama sheria namba nane ya mwaka 2007 ya mipango miji ingefuatwa kusingekuwa na
ujenzi holela nchini.
Pamoja na hayo Prof. Tibaijuka amesema
kwa kupitia mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa ifikapo mwaka 2017 kila
kipande cha ardhi kitakuwa kimepimwa.
KITAIFA
Makamu
mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Philip Mangula amesema kituo
hicho kimekumbwa na mpasuko baada ya vyama vya upinzani kususiakikao
kilichoitishwa Jumapili iliyopita.
Kitendo cha vyama hivyo kutoonekana kumetafsiriwa kama
mwendelezo wa kile kilichotokea katika Bunge Maalumu la Katiba Aprili 16, baada
ya wapinzani kususia vikao kutokana na kutokuridhishwa na mwenendo wa chombo
hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za
makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma Bw. Philip Mangula ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa
CCM, alisema kikao hicho kililenga kujadili mwenendo wa vyama na athari zake
kisiasa.
KIMATAIFA
Wapiganaji
wa Kiislamu wamedaiwa kuendelea kuteka
maeneo zaidi nchini Iraq, katika hatua ambayo Marekani imetaja kuwa ni tishio kwa eneo zima.
Polisi wa Iraq wamesema kwamba muungano wa
makundi hayo - Islamic State of Iraq na
Levant - ambao wanajiita kwa pamoja ISIS wameteka mikoa ya Kirkuk na Salehddin.
Inadaiwa kuwa wapiganaji hao
tayari wameteka mji mkuu wa pili kwa ukubwa nchini Iraq wa Mosul, Kaskazini
Magharibi mwa nchi hiyo.
Wanajeshi na polisi wanadaiwa kuwa wametoroka baada ya
makabiliano makali na wapiganaji hao wa kundi la Islamic State kutoka Iraq na
Syria, wanaojulikana kama ISIS, likiwa ni kundi lililochipuka kutoka Al Qaida.
Wapiganaji wa ISIS wamekuwa
wakisimamia shughuli za Mkoa wa Mosul kwa njia isiyo rasmi kwa miezi kadhaa
sasa, ambapo wametoza kodi kwa bidhaa zote zinazoingia na kuondoka eneo hilo na
wakati huohuo kupokea pesa za kutoa ulinzi kwa maafisa wa Serikali katika Mkoa
huo.
Majibizano ya risasi
yametokea katika meli iliyobeba wahamiaji haramu 300 katika ghuba ya Bengal na
kusababisha idadi isiyojulikana ya watu kujeruhiwa.
Meli hiyo
imekwama katika kisiwa cha Saint Martin, mji wa Teknaf ulioko wilaya ya Cox
Bazaar nchini Bangladesh.
Luteni Kazi Harunur Rashi wa kikosi cha ulinzi wa
pwani ya Teknaf amesema, walipewa taarifa kuwa meli hiyo imekwama baada ya
kupata ajali ikiwa na abiria 300 ambao walikuwa wanaelekea nchini Malaysia
kutafuta maisha bora.
Taarifa zaidi kuhusu uraia wa abiria hao na chanzo
cha majibizano ya risasi hazijapatikana.
Rais wa Sudan Kusini Salva
Kirr na kiongozi wa waasi Riek wamekubaliana kufanya mazungumzo ya kubuni
serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali wa nchi za mashariki na pembe ya Afrika
IGAD, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemarriam Desalegne, amesema kuwa uamuzi huo
umefikiwa kwa lengo la kukomesha vita huko Sudan Kusini.
Baada ya mkutano wa zaidi ya saa
nne katika ikulu ya waziri mkuu wa Ethiopia, mwenyeji wa mkutano huo
Hailemarriam Desalegne ametangaza kuwa Kirr na mwenzake Machar wako radhi
kushirikiana.
Ni kwa sababu hiyo vikao vitaanza
Addis Ababa baina ya washirika wa Salva Kirr, Riek Machar na wale kutoka katika
mashirika ya kijamii kujadili jinsi ya kuirejesha Sudan Kusini katika njia
ya amani.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa
viongozi hao wawili kukutana tangu watie mkataba wa kusitisha vita nchini Sudan
Kusini.
Shirika la IGAD ambalo limekuwa
likiongoza juhudi za upatishi katika mzozo huo uliodumu kwa miezi saba,
limeruhusu umoja wa mataifa kutuma vikosi vya usalama nchini Sudan kusini,
kulinda amani kama inavyohitajika kutoa ulinzi kwa waangalizi nchini humo..
0 comments:
Post a Comment