serikali ya malawi imesema kuwa itaimarisha uhusiano wake nan chi za china,india,na aafrika kusini ili kuimarisha uchumi wa taifa hilo pamoja na pato la taifa.
.........................................................................................................................................................
Hayo yamesemwa na Rais mpya wa Malawi Bw. Peter Mutharika ambaye alishinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 mwezi uliopita aliapishwa jana na kusema Malawi itahimiza uhusiano kati yake na China na Russia, ambao ni marafiki wapya.
Rais Mutharika amesema, katika kipindi chake atafanya juhudi zote kuhakikisha utulivu wa kiuchumi na umoja wa kitaifa, na pato la taifa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 7 kwa mwaka. Ameongeza kuwa, Malawi itaendelea na mawasiliano na nchi za magharibi ambazo zimeisaidia Mawali kwa muda mrefu, na itaendeleza uhusiano na marafiki wapya zikiwemo China, Brazil, India, Afrika Kusini na Russia