Mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.
Baro amekula kiapo hicho katika ubalozi wa
Gambia nchini Senegal huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi
zao.
Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh
amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi bw Jammeh kuondoka mamlakani.
Nje ya ubalozi huo raia wengi wa Gambia
wanaofanya kazi nchini Senegal wamekongamana kkushuhudia kuapishwa kwa rais
mteule wa Gambia Barrow ambaye wanamuona kuwa rais wa kwanza wa Gambia katika
kipindi cha miaka 22.
Kuapishwa kwa barrow wakati jammeh hajaondoka kutalifanya taifa hilo kuwa na viongozi wawili kwa cheo kimoja wakati barrow akitambuliwa kimataifa na rais jammeh akitambuliwa na bunge la nchi.
TAZAMA HAPA CHINI KUAPISHWA KWA BARROW.
0 comments:
Post a Comment