
Wengi wao walengwa wana shangilia kupost tu humu mitandaoni na wasijue ni nini hasa wanataka kiwe,
post zao za kusukuma siku iende na wasijue kiini chake nini hasa.
Hapo kale miaka ya 1900's watu walikuwa wanaadhimisha siku kama hii lakini sio ulimwengu mzima bali kwa mji MMoja wa New York.na Waliita SIKU YA KAZI WA WANAWAKE.na Hapo ikapiganiwa mpaka taifa zima lika kubali Mnamo 1908 na Kuifanya NWD(National Women's Day).
jumla ya wanawake 15,000 walikuwa wanakishinikiza ni kwanza wapate Mda Mfupi wa kufanya kazi,wawe na ujira mkubwa mahala pa kazi,na Haki ya kuchagua na Kuchaguliwa.
Na siku Hii waliiadhimisha Kila Juma la mwisho katika mwezi wa pili ambayo ilikuwa inawekwa tarehe 28.
Mapinduzi ya kusambaa kwa siku hii ni kutokana Dora ya Kirusi tena chini ya wafanyazi wa kiwanda cha nguo ambao ni wanawake walioandamana katika mji wa Petrograd siku hizi ni (Saint Petersburg),na hapa wanawake walishinikiza wawe na uwezo wa kujichagulia vitu vyao na sio kupangiwa.
maandamano yale yalipelekea serikali ya Mfalme wa Russia Nicholas II kujiuzuru na ikaja ya mpito iliyotoa nafasi ya wanawake kupiga kura .
kutoka hapo serikali ua Urusi ikaweka kila Tarehe 8 March Iwe siku ya mapumziko kitaifa na sherehe hii ya siku ya wanawakeilikuwa inategemea sana sherehe na harakati zaujamaa na nchi za kikomunisti mpaka ilipopitishwa mwaka 1975 na Umoja wa Mataifa kuwa siku ya wanawake Duniani..
MHIMU.
Na iwe chachu ya wanawake kufanya kazi kwa bidii tena Zilizo halali kwa Mjibu ya sheria za Nchi.
Marekani waliweka siku ya Kazi kwa ajili ya mwanamke,Huko Russia Waligoma wakiwa kiwandani wanawafanya kazi na sio vingine.
Kila Mwanamke yamfaa kuach UTEGEMEZI,dunia imewasikiliza na haki nyingi mmepewa nafasi yenu kuifanyia haki katika kazi na si kuwa wapokeaji tu,
By Mzee Wa Info Mjini Moshi,
0 comments:
Post a Comment