Hatimaye mgogoro wa ardhi baina ya jeshi la polisi Makambako wilaya ya Njombe na mama mjane Magreth Gumbo aliyekuwa anazuiwa kujenga nyumba katika kiwanja anachomiliki kihalali kwa madai kuwa amevamia eneo la jeshi makambako umepata ufumbuzi baada ya mkuu wa mkoa wa njombe Christopher Olesendeka kufika katika eneo hilo na kutoa maamuzi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe amefika katika mji wa Makabako kwaajili ya kufanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi na hapa ndipo kumeibuka suala la mgogoro wa ardhi wa muda mrefu uliokuwa unamkandamiza mama mjane kuzuwiwa kujenga katika eneo ambalo alipia serikalini tangu mwaka 2000 lakini anazuwiwa kujenga na kufanyiwa unyanyasaji na jeshi lapolisi.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi makambako sp peter kaiza amemuonyesha mkuu wa mkoa wa njombe mipaka ya eneo la jeshi la polisi pamoja na nymaba za wananchi wengine wanaodaiwa kuwa wamevamia eneo hilo
Baada ya kujionea hali halisi ya uonevu wa kumnyima haki mama mjane olesendeka amaetoa uamuzi kuwa mama huyo ajenge nyumba na asibugudhiwe pamoja na wengine waliko ndani ya eneo kulipwa fidia.
MSIKILIZE HAPA KWA SAUTI ZAIDI MWANDISHI WETU PROSPER MFUGALE KUTOKA MAKAMBAKO- NJOMBE
0 comments:
Post a Comment