MKOA Wa
Katavi umeteua siku ya jumamosi ya Kuwa siku Maalum kwa wakazi wa Mkoa huo
kufanya usafi Katika Mazingira yanayowazunguka.
Agizo hilo
limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dr Ibrahimu Msengi Wakati wa Uzinduzi wa siku ya Usafi Katika Mkoa wa Katavi
Ikiwa ni sehemu ya Kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
la Kufanyika usafi wa Mazingira ifikapo Decemba 9 Mwaka huu.
Dr Msengi
amesema amaagiza Viongozi wa ngazi ya Kata na Vijiji kuandaa utaratibu Maalum
wa Utekelezaji wa Agizo hilo ikiwemo Kuwachukulia hatu watu watakaokaidi agizo
hilo kwa Kushindwa kufanya usafi Katika Mazingira yanayowazunguka.
MKUU
WA MKOA WA KATAVI MSIKILIZE HAPA.
Wakati huo
huo Mkuu wa Wilaya Katavi Bw Paza Mwamlima ametangaza amri ya kila mtu
kuhakikisha anafanya Kazi ikiwa ni pamoja na Kuzuia bishara ya bar kufanyika
nyakati za asbuhi,Michezo kama pool table.
MKUUWA WILAYA YA MPANDA MSIKILIZE HAPA
.
Nao baadhi
ya wananchi walioshiriki Katika zoezi hilo la uzinduzi wa usafi wamemshukuru
Rais Dr John Pombe Magufuli Kwa uamzi wake wa Kusimamia usafi wa Mazingira
ambapo wamewataka Viongozi wenye Mamlaka ya kusimamia usafi wasisubiri amri ya
serikali ya juu na badala yake wafanye kazi zilizowajili.
Jumla ya
tani 65.4 za taka ngumu hukusanywa Katika Manispaa ya Mpanda hali inayochangia
kuwepo Kwa maeneo yenye uchafu sugu Katika Mji wa Mpanda.
0 comments:
Post a Comment