MKURUGENZI Wa Masnipaa ya Mpanda Bw.Suleiman Lukanga na
Watendaji Wengi wa halmshauri hiyo wamesimamishwa Kazi Kutokana na tuhuma za
Upotevu wa Shilingi Milioni 92.75.
Uamuzi huo Umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahim
Msengi Kutokana na Uchunguzi wa tume
tatu zilizoundwa Kuchunguza Upotevu wa Fedha hizo Kati ya Shilingi Milioni
200 Zilizotolewa na Tamisemi Kwa lengo
la Kununulia gari la Kubebea taka Katika Manispaa ya Mpanda.
Watendaji wengine Waliosimamishwa Kazi ni Kaimu Mkurugenzi
Bw.Vicent Kayombo ambae Pia ni Afisa Elimu Msingi Katika Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda, Afisa Manunuzi Bw,Kakulima Afisa Mipango, Bw Ferdinad
Filimbi Mweka hazina, Bw Bosco Kapinga, Mhasibu Kibi Hamis Msaka na Wajumbe wa
Bodi ya Zabuni.
MSIKILIZE KAMANDA WA POLISI KATAVI AKITHIBISHA KUKAMATWA KWA MMOJA WAO KWA MAHOJIANO ZAIDI
Katika Uchunguzi Uliofanywa na Kamati zilizoundwa chini ya
Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa Takukuru wamebaini Kuwa Kampuni ya Bluecyon iliyoko Mbezi Jijini Dar es
Salaam iliyopewa tenda ya Kununua gari hilo haifanyi Biashara ya Magari badala
yake ni Kampuini ya Uchapishaji yaani (Printing)
0 comments:
Post a Comment