Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ally Mohamed Shein atazindua kesho mbio za mwenge wa Uhuru katika sherehe zitakazofanyika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma imethibitisha leo kuwa Rais Shein atakuwa mgeni rasmi wakati wa zoezi hilo la kitaifa na imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa shughuli hiyo.
Pindi ukizinduliwa, Mwenge wa uhuru utakimbizwa mamia ya maili katika maeneo yote nchini sanjari na uzinduzi wa miradi ya maendeleo na kuhimiza mshikamano wa taifa kupitia hotuba na ushajihishaji.Sherehe hizo zinafanyika wakati wakosoaji wa mbio hizo za mwenge wa uhuru wakionya juu ya matumizi makubwa ya fedha za kufanikisha mbio zake ikilinganishwa na gharama za miradi inayozinduliwa.
Hata hivyo serikali mara kadhaa imepuzaa kauli hizo na kusema kuwa mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhai wa taifa
CHANZO CHA HABARI,,,https://www.facebook.com/301458400042694/photos/a.302006226654578.1073741828.301458400042694/361954953993038/?type=1&theater
0 comments:
Post a Comment