Tanzania Anthem

Sunday, 15 March 2015

WANAWAKE NDO CHANZO CHA UKIMWI

Na Isaack Gerald-Kataviimages Imeelezwa kuwa kundi la wanawake ndilo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka maambukizi ya virusi vya Ukimwi ukilinganisha na makundi mengine.
Hayo yamebainishwa leo na viongozi wa kamati za kupambana na Ukimwi Kata za Mpanda hotel,Uwanja wa ndege,Nsemulwa na Kichangani zilizopo Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoani Katavi wakati wakizungumza na Mpanda Fm/Mtandandao huu.
 Sanjari na hayo kamati hiyo imetaja sababu ya wanawake kuongoza kusababisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi tofauti Na makundi mengine kuwa ni kutokana na kushawishika kiurahisi na hatimaye kushiriki ngono zembe zisizo salama. Aidha kamati hizo zimeshauri elimu ya kijikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutolewa kwa watu wote bila kusahau watoto waliopo shuleni na nyumbani ili kupunguza asilimia 5.9 ya maambukizi iliyopo Mkoani Katavi. 

 Maambukizi ya virusi vya ukimwi huongezeka kutokana na  sababu mbali mbali ambazo huchangiwa wakati mwingine na uduni wa maisha,kushiriki ngono zembe,kutokuwa waaminifu katika mahusiano pamoja na kutumia dhana ambazo ni hatarishi na zimetumiwa na waathirika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive