Tanzania Anthem

Friday, 13 March 2015

POLISI VS BODABODA NJOMBE HAPATOSHI.

Madereva Wa pikipiki katika uwanja wa kituo kikuu cha polisi ,mkoa wa njombepicha na maktaba..
Polisi mkoani Njombe inaendesha msako mkali wa kuwakamata madereva wa pikipiki kufuatia matukio mawili yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita likiwemo la kuvamia kituo kikuu cha polisi Mjini Njombe tukio lililosababisha uvunjifu wa amani.

Kwa siku ya tatu mfululizo polisi inawatia nguvuni waendesha pikipiki pamoja na vyombo vyao vya moto na wengi waliokamatwa wamefikishwa kwenye kituo cha polisi mjini Njombe.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe Fulgensi Ngonyani amesema operesheni hiyo itaendelea hadi watakapofanikiwa kuwakamata wote waliohusika na matukio hayo na ameweka hakikisho kuwa askari wa jeshi hilo watazifikia pia wilaya za mkoa wa Njombe kuwabaini wahalifu.

Hata hivyo operesheni hiyo imetatiza huduma za usafiri kwenye Mji wa Njombe na wakazi wa eneo hilo wameihimiza polisi kufikisha kikomo msako huo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive