
Na issack Gerald_Katavi
Jeshi la Poliasi Mkoani Katavi limesema litaendelea kushirikisha jamii kwa ujumla katika kupambana na uharifu.
Hayo yamebainishwa leo na Kamishna msaidizi Mkoa wa Katavi Rashid Mohamed wakati wa mahojiano na Mpanda fm radio/mtandao huu Ofisini kwake
.
Aidha Kamanda Mohamed amezungumzia suala la watu wanaohamia katika mkoa wa katavi ambao inasemekana kuwa ndiyo wanaohusika na uharifu na kuwataka kuanzia serikali za mitaa mpaka Mkoa wanatakiwa kuwa na ushirikiano wa pamoja kupambana na uharifu mbalimbali ukiwemo unyang’anyi na udokozi wa vitu vya samani katika makazi ya watu.
Katika hatua nyingine akizungumza leo kwa njia ya simu na Mpanda radio Nestory Valentino Zacharia ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Airtel amesema kuwa wanakusudia kumwita Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bwana Pazza mwamlima Jumapili au jumatatu ijayo kuendesha zoezi la kupiga kura katika mtaa huo kuwapata waharifu kutokana na uharifu na uonevu wa baadhi ya nyumba kuendelea bila kukoma ikwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi kwa pamoja kutoa maamuzi dhidi ya waharifu watakaobainika kupitia upigaji kura.
Mara kadha sasa Mpanda Fm na mtandao huu imekuwa ikiripoti matukio mbalimbali ya uharifu ikiwemo mitaa ya airtel ambayo imekithiri katika mtaa huo na mitaa ningine ambapo sasa inaonesha dalili za kupoteza amani iliyopo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa katavi suala ambalo halitakiwi kufumbiwa macho.
0 comments:
Post a Comment