Na Stanley Msigwa_Mpanda
Rais Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete Ametaka Kuundwe Kwa Kamati Maalumu Kutoka Upande Wa Serikali,Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Pamoja Na Jukwaa La Tiba Asilia,Ili Kuhakikisha Kamati Hiyo Ishughulikie Matukio Ya Utekaji Nyara,Na Mauaji Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Yanayoendelea Nchini.
Akizungumza Na Mpanda Fm Radio/Mtandao huu Mwenyekiti Wa Jukwaa La Tiba Asilia Bonvetura Mwalongo,Aliyekuwa Ni Miongoni Mwa Wajumbe Waliokutana Na Rais ,Kwa Niaba Ya Mwenyekiti Wa Ujumbe Huo Na Mwenyekiti Wa Chama Cha Walemavu Wa Ngozi,Ernest Kamaya Ambapo Ameeleza Hali Ilivyokuwa Na Jinsi Gani Walifikia Maazimio Na Mheshimiwa Rais.
Aidha Bwana Mwalongo Amesema Kuwa Kufuatia Vurugu Hizo Ili Lazimika Usalama Wa Taifa Kuingilia Kati Na Kuwatoa Wote Ambapo Wale Waliolengwa Kuonana Na Mheshimiwa Raisi Wakarejea Kwa Wakati Mwingine.
Sanjari Na Hayo Lengo Kuu La Chama Cha Walemavu,Pamoja Na Jukwaa La Tiba Asilia Kukutana Na Mheshimiwa Rais Ni Kutaka Madai Yaliyopo Mahakamani Yashughulikiwe Mapema,Na Uboreshwaji Wa Utoaji Huduma Kwa Tiba Asili.
Kamati Hiyo Ya Pande Tatu Inatarajiwa Kutangazwa Kuanzia Jumatatu Ya Tare 9 Mwezi Huu Mara Baada Ya Tume Pande Zote Kukutana Na Mh.Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Wakati Huo Huo Kamati Ya Udhibiti Wa Vitendo Vya Utekaji Nyara Na Mauaji Ya Walemavu Wa Ngozi,Ikitaraji Kuundwa ,Wadau Na Wanaharakati Wanaojihusisha Na Utetezi Wa Walemavu Wa Ngozi Wameipongeza Hatua,Ya Mahakama Mkoani Mwanza Kuwahukumu Watu Wanne Adhabu Ya Kifo Baada Ya Kukutwa Na Hatia Ya Mauaji Ya Mwanamke Zawadi Magindu Mlemavu Ambapo Miongoni Yumo Mume Wa Mwana Mke Huyo.

ViCk Ntetema Ni Mwenyekiti Wa Asasi Inayojihusisha Na Utetezi Wa Masuala Ya Albino Ya Under The Same Sun, Ambapo Ameelezea Wao Kama Asasi Inayojihusha Na Upambanaji Huo Ni Jinsi Gani Wameipokea Hukumu Ya Mahakama.
"sisi kama wanaharakati na watetezi wa masuala ya albinism tumefurahi sana kutolewa kwa hukumu hiyo,kwani ni fundisho kutokana na mama huyo kuonewa sana,Si tu kwamba Aliuawa kikatili bali hata kaburi lake lilikuwa likifukuliwa na kubebwa mifupa yake,kwa hiyo hili linatakiwa kuwa la mfano".Alisema
0 comments:
Post a Comment