Tanzania Anthem

Tuesday, 17 March 2015

MARUFUKU KUTUMIA MTO KASIMBA TENA!!!

MAJINa Stanley Msigwa_katavi
Wakazi wa mitaa ya Msasani,Tambuka reli na Majengo Mapya katika halmashauri ya mji mpanda wametakiwa kuwazuia na kutowaruhusu watoto kuogelewa na kucheza katika maji yanayo tiririka kwenye mto kasimba.

Akizungumza na kituo hiki/mtandao huu mwenye kiti wa mtaa wa msasani Bwana Gerald Mboyi ,amesema kuwa kwa maji yanayotiririka katika mto huo si salama,na kwa mda mrefu mto huo umekuwa na madhara kwa kuwadhuru wakazi hao hususani wakati wa masika ambapo hujaa maji.
‘’natoa ilani kuanzia hivi sasa kwa mwananchi au mzazi yeyote haijalishiwa msasani,tambuka reli au majengo mapya ni marufuku kwenda kufua wala kuogelea katika maji yam to kasimba kwasababu si salama kiafya na vile vile yana madhara makubwa,kwani mwishoni mwa mwaka jana kuna mtu alipoteza maisha kwa kutumbukia laikini vilevile kuna watu wengi wanapoteza maisha kupitia mto huo,viongozi wa mitaa yote tushirikiane kulisimamia hilo ili tuweze kukomesha kabisa tatizo hiloAlisema.
Mto wa kasimba ni kiunganishi cha wakazi wa mtaa wa msasani na majengo mapya na ni kiunganishi kutokea eneo la mpanda hoteli kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa katavi na mkuu na ofisi ya mkuu wa wilaya yam panda kwa kupitia daraja la mto.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive