Tanzania Anthem

Tuesday, 24 March 2015

WALA FAINI KWA KUPANDISHA NAULI>>

basiNa Stanley Msigwa-katavi
mamlaka ya usafirishaji nchi kavu na majini SUMATRA Mkoa wa Katavi Imelitoza basi La A.N linalofanya Safari kati ya Katavi na Tabora faini ya zaidi shilingi laki saba kwa makosa matatu tofauti,likiwemo la kupandisha nauli.
Akizungumza na mpanda radio fm/mtandao meneja wa SUMATRA Bwana Aman Erasto amesema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T-810 AQY lilikiuka sheria kwa kujaza abiria kupita kiasi,kupandisha nauli zaidi ya bei elekezi na kufanya safari nje na ratiba.

Kwa upande wake bwana Thobiasi Joseph Msimamizi wa Magari ya Kampuni ya Zackaria Express Ameitaka SUMATRA kuangalia miundo mbinu kabla ya kuwatoza faini kwani miundo mbinu ndio chanzo cha wao kuvunja sheria.

Nae bwana masanja mwanaharakati NI miongoni mwa abiria waliokutwa na mkasa wa kupandishiwa nauli amesema kuwa kitendo kilichofanywa na SUMATRA mkoani katavi ni uvamizi kutokana na mamlaka hiyo kutangaza kushusha bei za mafuta na sio nauli.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive