Mkoa wa Katavi umepeleka vifaa mbalimbali vya kufundisha na kujifunzia katika shule ya msingi Azimio kitengo maalumu cha watoto wenye ulemavu.
Akizungumza jana na Mpanda fm Ofisini kwake,kaimu Afisa elimu Mkoa wa Katavi Saidi Mwapongo amesema kuwa vifaa hivyo vilipokelewa tangu mwishoni mwa mwaka jana kutoka serikali kuu kupitia Wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi ni pamoja na Alphabet block 6,Styus Block 6,jeometri set 6 na drawing Tool 6 vyote vikiwa vimepelekwa shule ya msingi Azimio .
Hata hivyo kwa mjibu wa Mwapongo,shule ya watoto wenye ulemavu iliyopo Majimoto Wilaya ya Mlele ipo katika hatua nzuri ya ujenzi wa miundombinu ya mabweni na madarasa ya wasichana na wavulana ili kutengeneza mazingira rafiki kwa aina zote za watoto wenye ulemavu ikiwemo ulemavu wa viungo.
Lakini pia Saidi Mwapongo anabainisha baadhi ya changamoto zinazokabili kitengo cha watoto wa shule wenye ulemavu kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia na uhaba wa walimu wenye vitengo maalumu ambapo ahata hivyo amezishauri halmashauri kuwaruhusu walimu wanaohitaji kusomea vitngo hivyo kwenda kusoma.
Naye Mwalimu mkuu msaidizi katika shule ya msingi Azimio Joseph Lymond akizungumza na Mpanda Radio Fm,amesema tayari wamepokea taarifa kutoka ofisi ya Halmashauri ya Mji Mpanda kuhusu upatikanaji wa vifaa hivyo licha ya kwamba haijajulikana ni vifaa vya aina gani.
Aidha pamoja na mambo mengine,mwalimu Lymond amesema kupatikana kwa vifaa hivyo kutaongeza ufanisi katika ufundishaji na kupatikana kwa matokeo mazuri ya wanafunzi kitaaluma.
Hata hivyo shule za vitengo maalumu vya watoto wenye ulemavu Mkoani hapa zikiwemo Shule ya msingi Nyerere,Katumba iliyopo Nsimbo bado zinakumbwa na baadhi ya changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
0 comments:
Post a Comment