Tanzania Anthem

Monday, 23 March 2015

MAHELA:UBOVU WA MASOKO CHANZO CHA KUPACK KIHOLELA


Na Stanley Msigwa_katavi.

Muonekano Mbovu Na Kutoboreshwa Kwa Soko Kuu La Mkoa Wa Katavi Zimetajwa Kuwa Ni Sababu Zinazopelekea Uegeshaji Holela Wa Vyombo Vya Usarifishaji Pamoja Na Vuruguru Baina Ya Waegeshaji Hao.

Akizungumza Na Kituo Hiki Mwenye Kiti Wa Soko Kuu La Mkoa Wakatavi Lililopo Eneo La Kashaulili Mjin I Mpanda Bwana Aman Mahela Amesema Kuwa Mpka Hivi Sasa Bado Hawajaafikiana Na Halmashauri Ya Mji Kuona Ni Jinsi Gani Soko Litaboreshwa Na Kuweka Taratibu Wazi Kwa Watumiaji.
Aidha Bwana Mahela Kufuatia Vurugu Ambazo Hutokea Mara Kwa Mara Baina Ya Waendesha Vyombo Vya Usafirishaji Na Wafanyabiashara,Amewataka Waishi Kwa Kuheshimiana Na Watambue Kuwa Kila Mmoja Yupo Kwa Ajili Ya Kutafura Ridhiki.

“Naomba Tuishi Kwa Kuheshimiana Na Kila Mmoja Atambue Kuwa Kazi Ya Mwenzake Ina Umhimu Kama Ilivyo Kazi Yake Kwani Soko Hili Linatumiwa Na Kila Mtu Na Kila Mmoja Wetu Anapata Kitu Cha Kumuwezesha Yeye Na Familia Yake”.

Nao Wasukuma Mikokoteni Wametoa Malalamiko Yao Dhidi Ya Kile Wanachodai Kuonewa Na Wafanya Biashara Na Wamiliki Na Waendeshaji Wa Vyombo Vingine Vya Usafiri.

Sisi Tunapack Miferejini Kabisa Lakini Kinacho Kuja Kutukwaza Pale Madereva Wa Tax Na Bodaboda Kugoma Kutupisha Tukiwa Tunataka Kupakia Tunaambiwa Ondokeni Mkapakilie Huko,Na Ukizingatia Huyo Mtu Hana Uhalali Wa Kuapack Hapo”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive