Tanzania Anthem

Tuesday, 3 March 2015

WAKAZI WA MTAA WA AIRTEL WAPIGWA MAWE USIKU


Na Isaack Gerald-Mpanda fm Radio
PICHA NA MAKTABA

Imeelezwa kuwa kukithiri kwa vitendo vya uharifu katika kata za Nsemulwa na Uwanja wa ndege katika halmashauri ya mji Mpanda kunasababishwa na baadhi ya raia wanaohamia katika maeneo hayo bila utaratibu wa kufahamika wanakotokea.

Hayao yamebainishwa leo na polisi kata wa kata za Nsemulwa na Uwanja wa ndege Paschal Tungu wakati akizungumza na Mpanda fm pamoja na mtandao huu kuhusu kukithiri kwa vitendo vya wizi na udokozi wa mali za raia wakati wa usiku.

Msikilize hapa polisi kata paschal Tunguakielezea kuthiri kwa uhalifu

Alipoulizwa kuhusiana na nyumba za raia zinazosemekana kufanyiwa vurugu kwa kurushiwa mawe kamanda Tungu Alikuwa na haya juu ya sababu za vurugu hizo.

Msikilize hapa polisi kata paschal Tungu akielezea sababu ya nyumba kupigwa mawe.

Juhudi za Mapanda Fm Radio na Mtandao huu za kupata baadhi ya kaya zinazokumbwa na dhoruba ya kurushiwa mawe zligonga mwamba kutokana na wengi kuwa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutafuta riziki.Lakini kwa mjibu wa kamanda wa polisi kata,wafuatao ni Waathiriwa wa Tatizo Hilo Kama Alivyo wataja''.ZAINABU HASAANI,DATIVA KARUME MTEGA wakazi wa mtaa huo,Huku Wanaoshukiwa ni WINFRIDA JOHN(mkazi) na,CHARLES REVOCATUS Mwanafunzi wa Kidato Cha Pili Katika Shule ya Sekondary Nsemulwa Mjini Mpanda"Alisema

Si Mtaa wa Airtel Pekee unaosumbuliwa na vitendo vya uharifu vikiwemo wizi,unyang’anyi wa mali za raia na udokozi majumbani bali mitaa mbalimbali Mkoani Katavi inahitaji kufanyiwa oparesheni ya tokomeza uharifu ili mwananchi abaki salama wakati huo mwananchi yeye mwenyewe akitakiwa kuwa namba moja kuota ushirikiano kwa kwa jeshi la polisi kuwabaini wahusika ili wafikishwe katika mikono ya sheria.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive