
wakuliama watumbaku wakiwa kwenye hatua ya ukaushaji wa tumbaku,Picha na maktaba.
Na Agness Mnubi-Katavi
WAKULIMA wa zao la Tumbaku Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kupanda miti ya kutosha ili kuhifadhi mazingira.
Wito huo umetolewa na Bwana shamba kutoka kampuni ya Premium Idd Ramadhani wakati akihojiwa na Sauti ya katavi kuhusu athari za Uharibifu wa Mazingira zitokanazo na wakulima wa Tumbaku.
Kwa Mjibu wa Maelezo ya Bwana Ramadhani amefafanua kuwa Kilimo cha tumbaku huhitaji Kiwango kikubwa cha Matumizi ya Miti hivyo wakulima wa zao hilo wanatakiwa Kupanda Miti ya Kutosha ili kutunza Mazingira.
“bila miti zao zima la tumbaku halitawezekana,hivyo niwajibu wao sasa kupanda miti kwakua tumbaku bila miti haistawi,kwanza ni kwa ajili ya kukaushiana pia kwa ajili ya kulinda mazingira hivyo basi ni lazima wachukue jukumu la kupanda miti”
Bwana Ramadhani Akaongeza kuwa kila mkulima wa Tumbaku anatakiwa kupanda miti kuanzia 550 kwa mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Biashara ya miti , panda miti uongeze kipato cha familia na hifadhi mazingira
0 comments:
Post a Comment