Tanzania Anthem

Thursday, 5 March 2015

ZITTO:NGELEJA ANASEMA UPUUZI,NA STORI NYINGINE KUBWA ZA LEO SOMA HAPA>>

Mwenyekiti  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serilali (PAC) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, kwamba naye amekuwa akipokea misaada mbalimbali kwa matumizi binafsi kuwa ni upuuzi.



Zitto alijibu tuhuma hizo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, ikiwa ni siku moja baada ya Ngeleja kumtuhumu na kueleza kuwa tuhuma hizo ni za kipuuzi na kwamba ameshawahi kuzijibu huko nyuma na kuziita ni siasa za majitaka.

“Tuhuma zote hizo zimeshawahi kutolewa huko nyuma, hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka, hata hivyo zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo”.


“Watuhumiwa wa ufisadi wa Escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa, hivyo wanajaribu na wataendelea kubwabwaja na kuhangaika ikiwamo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao.”



“Ndiyo maana Ngeleja ametaja msururu wa watu akiwamo mfanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila kuwapo chembe ya ushahidi, hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke katika vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza,” Zitto.


Aidha, Zitto aliunga mkono kazi iliyofanywa na Baraza la Maadili, alieleza kazi hiyo ilipaswa kuwa imefanywa kwa muda mrefu sasa kwa kashfa mbalimbali zilizowahi kuwapata viongozi, kama vile rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya umeme, kujipatia mikopo katika taasisi za umma bila kulipa na kujilimbilikizia mali tofauti na kipato.

Zitto aliiomba Sekretarieti ya Maadili izichukulie kwa uzito tuhuma za Ngeleje dhidi yake, kwani kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma yanapaswa yafanyiwe uchunguzi.

Akijitetea juzi kwenye Baraza la Maadili, Ngeleja alikiri kupata mgawo wa Sh. bilioni 40.2 kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalila wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd na kudai kuwa wabunge wamekuwa wakifadhiliwa na wafanyabiashara na  mmoja wa wabunge walionufaika na misaada ya fedha za wafadhili, ni Zitto, ambaye kisheria ni mtumishi wa umma.

NIPASHE

Taifa limekumbwa na msiba mkubwa, baada ya watu 38 kufa na wengine zaidi ya 82 kujeruhiwa vibaya, baada ya kuangukiwa na nyumba zilizobomolewa na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana ikiambatana na kimbunga, katika kijiji cha Mwakata, kata ya Isaka, wilayani hapa, mkoa wa Shinyanga.

Kufuatia maafa hayo, Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi na pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nasoro Rufunga, kuomboleza vifo vya watu 38 na pole kwa wengine 82 waliojeruhiwa.

“Nimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 38 waliopoteza maisha na wengine 82 waliojeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu baada ya nyumba zao kusombwa kabisa na maji kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha,”.

Rais Kikwete katika salamu zake kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano  ya Rais Ikulu, alisema msiba huo siyo wa wananchi wa Shinyanga pekee, bali ni wa Taifa zima ambalo limepoteza nguvukazi muhimu kwa maendeleo yake na ustawi wa jamii.

Aliwaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira wakati huu wa majonzi makubwa kwao wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao na wasisahau ukweli kwamba kazi ya Mungu haina makosa.

Aidha, aliwahakikishia wafiwa wote kuwa binafsi yuko pamoja nao katika kipindi chote cha kuomboleza msiba huo mkubwa kwao na kwa Taifa.

Maafa hayo yalitokana na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali na hivyo kuathiri watu 3,500.

Alivitaja vijiji vilivyoathirika kuwa ni, Makata ambako kaya 350 zimeathiriwa, kijiji cha Ngumbi, kaya 100 zimeathirika na katika kijiji cha Magung’hwa, kaya 50 zimeathiriwa.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, akizungumzia tukio hilo, alisema idadi ya watu waliokufa wengi wao ni watoto ambao walisombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua hizo baada ya maji kujaa ndani ya nyumba na kubomoa nyingine.

Kamugisha alisema idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na waokoaji kuendelea kufukua vifusi vya nyumba zilizobomoka.

Alisema hadi sasa majina ya waliokufa hayajafahamika kutokana na kuendelea kwa kazi ya uokoaji.

“Tunaendelea na uokoaji na kufukua miili ya watu pamoja na madhara mengine yaliyopo, idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka… Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga itakutana baadaye ili kutathmini maafa hayo pamoja na kujua msaada upi unahitajika kwa waathirika,” Kamugisha.

Alisema mvua hiyo ilianza kunyesha saa 4:00 usiku wa kuamkia jana na kudumu kwa saa kadhaa na kusababisha maafa hayo.

NIPASHE

Meneja Miradi ya umeme ya Kinyerezi, Simon Jilima, amesema mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia  kukamilika mapema  Juni mwaka huu.

Jilima aliyasema hayo mbele ya  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  iliyofanya ziara katika mtambo  huo  ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara  ya kutembelea miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida,  Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini aina ya tanzanite katika mkoa wa Manyara.

Jilima alisema kwa sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 na kufafanua kuwa kazi inayofanyika kwa sasa ni kumalizia utandazaji wa nyaya, ufungaji wa mabomba ya maji na gesi  pamoja na ujenzi wa barabara za ndani.

Alisema ofisi kwa ajili ya watumishi pamoja na  karakana kwa ajili ya kuhifadhia mitambo imekamilika.

Jilima alisema mpaka sasa serikali imelipa kiasi  cha Dola za Marekani milioni 167.2 na  kuongeza kuwa  kiasi cha  Dola za Marekani milioni 15 kinatarajiwa kumaliziwa kabla ya kukamilika kwa mradi.

Jilima alieleza kuwa awali changamoto kubwa ilikuwa ni  ukamilishwaji wa mradi wa bomba la gesi ili waanze kutumia gesi hiyo katika kuzalisha umeme, lakini kutokana na kasi  ya mradi huo kuwa ya kuridhisha, wana imani kuwa gesi itaanza kuzalishwa mapema  kabla ya kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi 1


“Ndugu wajumbe, awali tulikuwa na wasiwasi wa kupatikana kwa gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kupitia mradi wa Kinyerezi 1 kutokana na mradi wa  bomba la gesi kuwa na changamoto nyingi, lakini baada ya kuona  mradi wa bomba la gesi uko katika hatua nzuri yaani zaidi ya asilimia 90, tunaamini kuwa  mara mtambo utapokamilika, gesi itakuwa imekwishaanza kuzalishwa na hapo ndipo tutaanza kuzalisha  umeme mara moja,” Jilima.


JAMBOLEO


Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia FFU Mkoani Mwanza PC Magesa ameuawa baada ya kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Kamanda wa Polisi Mwanza,kamishna msaidizi mwandamizi ‘SACP’  Valentino Mlowola alithibitisha jana ni kweli askari huyo ameuawa.

Askari huyo akiongozwa na polisi jamii walikwenda eneo la tukio usiku kwa nia ya kuwakamata watu hao wanaodaiwa kuwa ni wezi wa mafuta,lakini baada ya kupata taarifa walijipanga ili kutelekeza unyama huo.

“Inaonyesha askari polisi akisaidiwa na polisi jamii walikwenda kutekeleza jukumu hilo kinyemela na walipofika eneo la tukio ambapo uhalifu ulitokea walifanikiwa kuwakamata baadhi ya wahalifu”:-Mlowola.


“Lakini gafla walijitokeza wengine kasha kuwazingira na wakamuua askari wa FFU kwa kumnyonga shingo”.


HABARILEO


Mnikulu Shaban Gurumo amekiri mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, kwamba alipokea Sh milioni 80.8 kutoka kwa James Rugemalira na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi, ingawa amekanusha kuomba fedha hizo.

Gurumo alitoa utetezi huo jana Dar es Salaam mbele ya baraza baada ya kusomewa mashitaka ya kutumia cheo chake cha uongozi wa umma vibaya na kujipatia fedha hizo, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Alikiri kumfahamu Rugemalira, akisema ni rafiki yake kwa zaidi ya miaka 10. Alisema.. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive