Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa
kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia
ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa
huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa
kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na
kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye
mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na
upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo
viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
SOURCE:NIPASHE
SOURCE:NIPASHE
0 comments:
Post a Comment