Tanzania Anthem

Friday, 20 March 2015

MSENGI:LAZIMA WOTE WARUDI SHULENI.

Ibrahim-Msengi
Mkuu wa Mkoa Wa Katavi,Dr Ibrahim Msengi,Picha na Maktaba

Na Meshack Ngumba-Katavi

 MKUU wa Mkoa wa Katavi Dokta IBRAHIMU MSENGI ameagiza Wanafunzi waliohitimu Elimu ya Msingi mwaka 2014 na kufaulu kwa kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari, waripoti katika shule walizopangiwa.
Dokta MSENGI ametoa kauli hiyo katika Hotuba yake iliyosomwa kwa Niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu ISSA SELEMAN NJIKU, wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi,Wataalamu wa Elimu Mkoani Katavi. Mkuu huyo wa Mkoa amehimiza kukomeshwa kwa Watoro Mashuleni Wanafunzi walioacha shule wasakwe, na kurudishwa shuleni ili waendelee na masomo.

kumekuwa na operesheni mbali mbali za kuwa rudisha wanafunzi watoro na walioacha masomo katika mkoa wa katavi,ambapo mkuu wa wilaya ya mpanda Bwana Pazza Mwamlima tarehe 12 february mwaka Huu alifanya msako rasmi wa kuwa saka watoro na kuwarejesha mashuleni ,ambapo kwa mjibu wa takwimu,
za ofisi ya mkuu wa wilaya zinaonesha kuwa kwa halmashauri ya mpanda mji ni zaidi ya watoto mia tisa waliacha masomo kwa sababu mbali mbali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive