Na isaack Gerald_katavi
Chama cha walimu (C.W.T) wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi watakaoongoza chama hicho kitengo cha wanawake kwa miaka mitano.
Viongozi hao ambao wamechaguliwa ni pamoja na Zuhura Selemani nafasi ya mwenyekiti,Sesilia Wihala nafasi ya Mhasibu,Gladness Godon,Theresia Mlolwa,Jovither Rwehumbiza na Donatha Vianey nafasi ya ujumbe wa chama.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo wa C.WT.ngazi ya Wilaya Kitila Kitundu pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wanaoingina madarakani kufanya kazi kwa ushirikano bila ubaguzi katika kutoa huduma kwa wahitaji kusaidiwa.
Wakati huohuo kiongozi wa CWT anayemaliza muda wake kitengo cha wanawake maarufu kama ke mwl.Anna Lais ,amewataka viongozi wanawake waoingia madarakani kuacha ubabe wa madaraka na badala yake watoe huduma kwa walengwa kama inavyotakiwa.
Aidha pamoja na mambo kadha wa kadha,mwalimu Lais pamoja na wajumbe wengine wa mkutano huo wa uchaguzi wameiomba ofisi ya utumishi Mpanda kuangalia kwa makini suala la unyanyasaji wa masuala ya wanawake yakiwemo masuala ya nafasi za oungozi wa ngazi za juu vilevile katika kutoa huduma kwa watumishi na wanachama wa chama cha CWT wanapohitaji kusaidiwa.
Hata hivyo wamepanga kufikisha baadhi ya masuala yao wanayoyahitaji kufanyhiwa kazi katika kikao cha mkutano mkuu wa uchaguzi wa wanaume ngazi ya Wilaya.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho cha walimu Wilaya ya Mpanda Willison Masolwa wakati akizungumza na mpanda fm ofisini kwake mapema leo ameakiri kuwepo kwa changamoto za unyanyasaji kwa walimu wanawake kama anavyobainisha
.
Aidha uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa Chama cha walimu C.W.T kwa wanaume ngazi ya Wilaya unatarajia kufanyika kesho katika ukumbi wa Romani Catholic kupitia mkutano mkuu wa Wilaya wa chama hicho.
0 comments:
Post a Comment