Tanzania Anthem

Friday, 27 March 2015

KUCHELEWESHWA KWA KESI CHANZO CHA SHERIA ZA MKONONI.

Na Isaack gerald-KATAVI
Imeelezwa kuwa chombo cha mahakama kuchelewa kuwajibika ipasavyo katika kutoa maamuzi ya ma
shauri katika mahakama Mikoa ya Rukwa na Katavi kumekuwa chanzo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi dhidi ya waharifu.

Hayo yamebainishwa leo na Jaji Mfawidhi Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Kakusulo Sambo katika kikao cha Balaza la wafanyakazi wa mahakama kanda ya Sumbawanga ambacho kimefanyika Mjini Mpanda.

Aidha,Jaji Sambo  amesema Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga imeweka mikakati ya kuamua mashauri yote yaliyopo mahakama za Mikoa ya Rukwa na Katavi kuanzia mashauri yenye miezi 18-miaka 10 ambapo yanatarajiwa kuamuliwa kuanzia mwezi machi mpaka mwezi Desemba mwaka huu.

Jaji Sambo ameongeza kuwa baada ya maazimio yaliyoafikiwa katika kikao cha majaji kilichofanyika Mkoani Mwanza mwezi Novemba mwaka jana ya kutochelewesha mashauri ya kesi,pia mwezi ujao majaji mafawidhi wa  mahakama nchini wanatarajia kukutana kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa maamuzi ya mashauri yaliyopo mahakamani.

Wakati huohuo taarifa ya Naibu Msajili Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga inaonesha Mahakama ya Wilaya ya Mpanda inaongoza kwa mashauri 438,ukilinganisha na Mahakama ya Wilaya ya Nkasi yenye mashauri 373 huku Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga ikiwa na mashauri 78 huo ukiwa ni wastani wa kesi kwa mwaka.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive