Na Agnes mnubi-katavi
Jumla ya watu 10,961 Mkoani Katavi wanaishi na Virusi
vya UKIMWI ikiwa ni takwimu za Mkoa kwa mwaka 2014.
Takwimu hizo Zimetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Katavi DKT GABRIEL CHENGULA wakati
akihojiwa na Sauti ya Katavi ofisini kwake ili Kujua takwimu za Maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi Mkoani hapa.
Dkt. Chengula amesema kuwa Idadi ya watu walioambukizwa
Virusi vya Ukimwi Mkoani KATAVI huongezeka Kila mwaka ambapo kwa mwaka 2013
idadi ya watu waliokuwa wameambukizwa
walikuwa 5,389.
Pia Dkt Chengula amesema sababu Kubwa ya Kuongezeka kwa
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kunatokana na watu Kutojitokeza Kupima ili
kujua afya Zao.
Aidha Chengula ameongeza kusema kuwa uhaba wa watumishi wenye
ujuzi , wagonjwa kutotumia dawa kwa usahihi kadri ya maelekezo waliyopewa,
kukatiza matumizi ya dawa pamoja na wagonjwa kuikataa hali yao ya ugonjwa ni
miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa kutoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Kiwango cha Maambukizi ya Ukimwi Katika Mkoa wa KATAVI Ni
asilimia 5.9 wakati wastani wa Taifa
Ukiwa ni asilimia 5.1
0 comments:
Post a Comment