Home »
New info
» KUJUA SHERIA ZA KANI NI MHIMU!! SOMA ZAIDI
Waajiri na waajiriwa wametakiwa kutambua haki zao katika
maeneo yao ya kazi ili kuepukana na matatizo yasiyo ya msingi yanayojitokezea
baina ya muajiri na muajiriwa
Akizungumza na kituo hiki mwezeshaji masuala ya ujasilia mali yanayofadhiliwa na
shirika la kazi duniani ILO Bwana Beny Mwambela amesema kwa sasa waajiri pamoja
na waajiriwa wanashindwa kutambua haki zao kutokana na kutozijua sheria za kazi
na ndio maana wameona kuna haja ya kumsaidia mjasiria mali mdogo.
Aidha Bwana Mwambela kumekuwa na uoga kwa waajiri pamoja na
waajiriwa juu ya haki zao za msingi
kutokana na kutozijua sheria za kazi
zinasema hivyo shirika la kaz duniani,pamoja na shirikisho la waajili nchini
likaona umhimu wa kumpatia semina hiyo mjasiria mali.
Kwa upande wao wajasilia mali waliohudhulia mafunzo hayo
wamewapongeza waandaji wa semina hiyo na kusema kuwa kwa sasa wanaamini kuwa
watapata haki zao na kuwa sheria nyingi walikuwa hawazijui kabla ya mafunzo
hayo.
0 comments:
Post a Comment