
Na Stanley Msigwa Chanzo jeshi la polisi
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma
limesema leo alfajiri vimeokotwa
vipeperushi maeneo mbalimbali mjini hapa vyenye ujumbe unao chochea uvunjifu wa amani.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polis David
Misime amesema wanaendelea kupata taarifa za watu wanao daiwa kuandaa
vipeperushi hivyo na wanalifanyia kazi
ili waweze kuwakamata na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa vitisho na
uvunjifu wa amani.
Aidha
kamanda Misime ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma na wageni waliopo
mkoani hapa watii sheria bila
shuruti kwa kuhakikisha kila mmoja
anajiepusha na uhamasishaji wa uvunjifu wa amani kupitia mikusanyiko isiyo
halali na maandamano ambayo yamekwisha pigwa marufuku.
Sanjari na
hayo amesema jeshi la polisi limejiimarisha ipasavyo kukabiliana na yeyote Yule
atakaye kiuka sheria na maelekezo yaliyo tolewa.
0 comments:
Post a Comment