Wakazi wa Manispaa ya Dodoma
wameulalamikia uongozi wa mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA kwa
kuwakatia maji ili hali wakijua wana hali ngumu ya kiuchumi.
.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi
hao wamesema wamekuwa wakipata changamoto kubwa katika ulipaji wa bili ya maji
kutokana na hali ngumu ya kiuchumi hali inayowapelekea baadhi yao kushindwa
kabisa kutoa mchango huku wengine wakitoa nusu ya fedha zinazohitajika.
Pia wakazi hao wameiomba Mamlaka
hiyo kuwavumilia pindi wanapochelewa kulipa bili kwani wanatambua umuhimu wa
maji lakini hali ngumu ya maisha ndiyo inayopelekea wao kushindwa kulipa kwa
wakati.
Kwa upande wake Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Maji safi na
usafi wa mazingira DUWASA Bi Angela Anton amesema wamekuwa wakiwaonea huruma
wananchi kutokana na hali ngumu ya maisha hivyo kuwavumilia katika ulipaji wa
bili ya maji lakini kwa sasa wameanzisha mkakati wa kuwakatia wale wote
waliolimbikiza bili kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Malalamiko haya ya wananchi
yanafuatia baada ya mamalaka ya maji safi DUWASA kuanzisha opareshen ya
kuwakatia maji au kuwang,olea mabomba wateja wote wenye malimbikizo ya madeni.
0 comments:
Post a Comment