Home »
New info
» NCHIMBI; MKOA WA DODOMA UMESHAMBULIWA NA MBWA VICHAA!!
Mkoa wa Dodoma na wilaya zake unakabiliwa na tatizo la
kuzuka kwa mbwa wenye ugonjwa wa kichaa wanaowadhuru wananchi na
kuwasababishia madhara makubwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi alipokuwa akizungumza na Dodoma FM katika Viwanja vya Nane nane ambapo amesema
mpaka sasa takribani watu kumi huripoti
hospitali kwa siku
kutokana na kuumwa na mbwa hao.
Hata hivyo Dr.Nchimbi
amewataka viongozi wa Halmashauri zote kuchukua
hatua za haraka kuwatangazia
wananchi wote wa mkoa wa Dodoma juu
ya kuzuka kwa wimbi
la ugonjwa wa Mbwa Kichaa ili
waweze kujikinga nao .
Pia ametoa agizo kwa
wamiliki wa mbwa hao kuwafungia mbwa wao na kuwapa chanjo mara kwa mara ili kupunguza madhara yatokanayo na ugopnjwa wa mbwa kichaa.
0 comments:
Post a Comment