Wakazi wa kijiji cha Hombolo Makulu Mkoani Dodoma wameilalamikia Serikali ya kijiji kwa
kushindwa kudhibiti tatizo la uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji .
Wakizungumza
na kituo hiki wakazi hao wamesema tatizo hilo la uharibifu wa mazingira limekuwa
likifanywa na watu wanaofahamika katika serikali za mitaa lakini uongozi
umeshindwa kulitatua kutokana na kuendekeza rushwa baina yao na waharibifu hao.
Aidha
wakazi hao wamesema kutokana na kukabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira
katika vyanzo vya maji kijijini hapo kunapelekea
mvua kushindwa kunyesha kwa wakati .
Kwa upande
wake Afisa Mifugo Mstaafu kijijini hapo Bw. Josephu Moleri amesema hali ya
mazingira ni mbaya kutokana na viongozi wa eneo hilo kuruhusu baadhi ya watu
kufyeka miti kando kando mwa vyanzo vya maji .
Akitoa
ufafanuzi juu ya tukio hilo Diwani wa kata ya Hombolo Bw Musa Kawea amesema tatizo
la uharibifu wa mazingira ni tatizo la Kitaifa hivyo serikali inapaswa kuongeza
maafisa misitu ili kupunguza tatizo hilo la uharibifu katika eneo hilo kwani
linakabiliwa na uhaba wa Maafisa Misitu.
0 comments:
Post a Comment