Wabunge wameendelea
kuishauri Serikali juu ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa ajili ya
kuwekeza katika maendeleo ya Taifa.
Akichangia mjadala wa Bajeti katika kipindi cha majadiliano
Bungeni mjini Dodoma Mbunge wa Kuteuliwa Bw.James Mbatia ameishauri serikali
iangalie namna ya kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Aidha Bw.Mbatia amesema kunavyanzo vingi vya mapato ambavyo
vinaweza kutumika vizuri katika kuongeza kipato na kuchangia kwa kiwango
kikubwa katika bajeti ya nchi.
Sanjari na hayo amewataka viongozi kuwa mfano bora kwa
kulipakodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo.
Na Pasko mwinje
Chanzo Bunge
Pamoja na Tanzania kupiga hatua kubwa katika kupunguza Maambukizi ya
Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama Kwenda Mtoto wananchi wametakiwa
kutokujibweteka.
Haya yamesemwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Dodoma Bi Rehema Madenge katika uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga
Maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa mama kwenda Mtoto ambapo amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza
maambukizi hayo.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Dodoma
Dr Ezekieli Mpuya amesema kiwango cha maambukizi mapya kitaifa
na katika mkoa wa Dodoma kipo juu ,ambapo serikali inashirikiana na nchi nyingine kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya.
Akielezea lengo la uzinduzi wa
Kampeni ya Kupinga maambukizi mapya Mkurugenzii uendeshaji wa Shirika la
Tunajali DR Joseph Ng’weshemi amesema
lengo ni kuhakikisha mtoto
anayezaliwa na mama mwenye maambukizi anazaliwa
akiwa salama.
Na Stanley Msigwa
Chanzo Dodoma FM
Imeelezwa kuwa Rushwa na Matumizi makubwa ya serikali pamoja
na bajeti tegemezi ni miongoni mwa maaudui
wa bajeti ya serikali hapa nchini.
Hayo yamesemwa na
Mbunge wa jimbo la Mwibala Bw. Kangi Lugola alipokukuwa akichangia
mjadala wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 ambapo ametanabaisha
kuwa maadui hao wasiposhughulikiwa bajeti nyingi hazitatekelezeka.
Aidha Bwana Lugola amesema pamoja na serikali kuwa na mpango
wa miaka mitano lakini bajeti zimekuwa
zikija tofauti na mpango huo hivyo kusababisha bajeti kutokutekelezeka.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalu kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )
Bw.Christowaja Mtinda amehoji ni kwanini
serikali haijachukua chanzo hata kimoja cha mapato kilichopendekezwa na kamati
ya Bajeti.
Na Lucas Godwin Chanzo
Bunge
KITAIFA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC inatarajia kutumia zaidi ya Sh. bilioni 298
kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa
teknolojia mpya ya Biometric Voter Registiration .
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva amesema uboreshaji
wa daftari hilo awamu ya kwanza unatarajia kufanyika Mwezi Agosti na Septemba
mwaka huu nchini kote.
Bw Lubuva amesema uamuzi wa kuanza
kutumia mfumo huo umefikiwa kutokana na changamoto zilizojitokeza katika
matumizi ya teknolojia ya Optical Mark Recognition ambao ulisababisha kwa kiasi
kikubwa daftari hilo kuwa na kasoro.
Na Stanley Msigwa
Chanzo Nipashe
KIMATAIFA
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema idadi ya raia wanaotafuta hifadhi
katika maeneo ya ulinzi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini sasa imefikia
elfu 95.
Akinukuu takwimu
kutoka tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Bw Dujarric amesema zaidi
ya watu elfu 30 wapo katika mji wa Juba na wengine elfu 38 wapo kwenye kituo
cha Bentiu wakati elfu 18 wapo Malakal huku
wengine wakiwa katika miji
mingine.
Amefafanua kuwa
maeneo mengi yaliyoanzishwa kwa ajili ya kuhifadhi watu wa nchi hiyo
yamekamilika au yanakaribia kukamilika, na huko Malakal watu elfu 7 tayari
wameshahamia katika maeneo mapya.
Wasiwasi nchini
Sudan Kusini unazidi kutanda na kugeuka kuwa mgogoro baada ya serikali ya rais
Salva Kiir kuwatimua wanajeshi wanaomtii makamu wa rais wa zamani Riek Machar
na kufanya jaribio la mapinduzi.
Na Zania Miraji
Sauti ya China
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa
Mataifa UNHCR, limesema idadi ya watu waliopoteza makao yao na kufanywa
wakimbizi kutokana na vita ni zaidi ya
milioni hamsini.
Idadi
hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya
dunia ambapo Takriban watu milioni 17 walitoroka nchi zao na zaidi ya milioni
thelathini ni wakimbizi wa ndani ya nchi zao.
Vita
nchini Syria, ni moja ya sabab ya kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi,
lakini pia kuna mizozo mingine katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Sudan
Kusini ambayo imechangia idadi kubwa ya wakimbizi.
Shirika
la kuwahudumia wakimbizi limesema kuwa
idadi hiyo ni ishara tosha ya athari za kukosa kuzuia mizozo ambapo limetaka
mataifa tajiri kufanya juhudi kuhifadhi
wakimbizi hao
Na Zania Miraji Chanzo
BBC
Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda,
Balozi James Mugume amesema Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na
Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu mapenzi ya jinsia moja.
Serikali
ya Uganda imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi
hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo
imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Kadhalika
msemaji wa serikali Ofwono Opondo amenukuliwa na shirika la habari la AFP
akisema kuwa wananchi wa Uganda wanafahamu kuwa hawatategemea tena msaada wa
nchi za Magharibi
Vikwazo
ambavyo vimetolewa na Marekani dhidi ya Uganda ni pamoja na kufutilia mbali msaada
wa kijeshi, kuwapiga mrufuku baadhi ya maafisa wa serikali ya Uganda kusafiri
nje na kupiga tanji mali zao.
Na Zania Miraji
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment