Tanzania Anthem

Friday, 20 June 2014

HIKI NDICHO WALICHOVUNA UGANDA MARA BAADA YA KUPINGA USHOGA


 Mara baada ya Uganda kupinga ushoga hiki ndicho watu wa magharibi walichosema.

Msemaji wa Whitehouse, Caltlin Hayden ameeleza katika barua yake kwa vyombo vya habari kuwa sheria iliyopitishwa na bunge la Uganda ikiuka haki za binadamu.


Vikwazo vya Marekani kwa Uganda kama adhabu, vinajumisha kuwapiga marufuku wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kutoingia Marekani.

Marekani itapunguza ushirikiano na Wizara ya Polisi na Afya za Uganda, na kuachana na mpango wa mazoezi ya kijeshi kati ya wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa Uganda.

Uganda walipitisha sheria ambayo inaeleza wazi mtu atakayekutwa na hatia ya kushiriki katika masuala ya ushoga atahukumiwa kifungo cha maisha jela.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive