DODOMA
Wakazi wa Kata ya
Hombolo Manispaa ya Dodoma wamelalamika
tatizo la uhaba wa maji safi linalo
wakabili kijijini hapo.
Wakizungumza na Dodoma fm wakazi wa kata ya Hombolo wamesema
upatikanaji wa Maji safi umekua mgumu kutokana na watu waliochimba visima na
mabomba kuuza maji hayo.
Nae Mwenyekiti wa
serikali ya Kijiji cha Hombolo Bw.Yared
Mtagwa ame kiri kuwepo kwa tatizo la maji kijijini hapo ambapo amesema serikali
ya kijiji ipo kwenye mpango wa kutatua
tatizo hilo.
Akizungumzia suala hilo Diwani wa kata ya Hombolo Bw.Mussa Kawea amesema
tayari jitihada zinafanyika na
tayari wamekwisha ongea na Wamisionari
ili wameweza kuwasaidia kufufua visima.
Na stanley Msigwa dodoma fm
Serikali
imeshauriwa kujipanga kwa kuboresha miundo mbinu ikiwemo barabara pamoja na
reli ili kupunguza mfumuko wa bei ya mazao nchini.
Hayo yamesemwa na mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania Bwana Gozbert Blandes alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya
serikali bungeni mji Dodoma ambapo
amesema mfumuko wa bei huchangiwa sana na bei ya vyakula.
Aidha Bwana Blandes ameishauri serikali kuhusiana
na fedha za tozo ya umeme vijijini ziwek we kwenye mfuko maalumu ili zifanye
kazi ya umeme vijijini kama serikali
ilivyokusudia.
Nae mbunge wa viti maalumu Cecilia Pareso
amesema suala la manunuzi ya uma hasa pale kunapokuwepo na warsha au semina
liangaliwe na lizibitiwe ili kuondoa ubadhilifu wa fedha za umma.
Serikali
imewataka wamiliki na waendesha magari ya mizigo kulinda bima zao kwa matumizi ya watu wengine barabarani.
Hayo yamesemwa na Naibu
waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba Wakati Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Mary Chatanda
lililohoji juu ya baadhi ya malori yanayofanya safari
zake kati yaTanzania na nchi jirani kukwepa
kulipa kodi kwa kulipa Bima bandia.
Aidha Waziri Nchemba amesema sheria
ya bima za magari ya mwaka 2002 inakataza gari lolote nchini kutembea
bila bima, na sheria ya bima ya mwaka
2009 inatoa adhabu kali kwa mmliki atakaebainika kujihusisha na utengenezaji au usambazaji wa Bima Bandia.
KITAIFA
Teknolojia
ya kisasa inayotumika katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukabiliana
na dawa za kulevya imeonyesha mafanikio katika kuwabaini wanaojishughulisha na
usafirishaji wa dawa hizo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa uchukuzi Dk Harrison
Mwakyembe wakati akifungua semina ya Baraza la Viongozi wa Dini la kupambana na
dawa za kulevya Tanzania iliyofanyika
jijini Dares salaam.
Aidha Dr.Mwakyembe amesema teknolojia hiyo imesaidia
kupunguza aibu ya watu wanaokamatwa na dawa za kulevya katika nchi nyingine
duniani kote wakitokea Tanzania .
Dk Mwakyembe amesema wizara yake ipo katika mchakato wa
kutafuta kampuni yenye teknolojia ya kisasa zaidi itakayoimarisha ulinzi na
kukabiliana na hila zote za wasafirishaji
ambapo ameaomba ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama ili kubaini
mtandao wa biashara hiyo.
KIMATAIFA
Kenya imesema haitaondoa majeshi yake nchini Somalia licha ya
kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa wapiganaji wa Somalia.
Naibu rais wa Kenya Bw
William Ruto akizungumza na waziri mkuu wa Somalia Bw Abdiweli Ahmed
amesema Kenya haiwezi kuacha majukumu
yake yanayoendelea nchini Somalia na kwamba itashirikiana na tume ya Umoja wa
Afrika nchini Somalia kuhakikisha kuwa utulivu unapatikana nchini humo.
Mbali na hayo habari
zinasema kuwa Kenya na Israel zimeahidi
kuimarisha ushirikiano kati yao kwenye mapambano dhidi ya ugaidi .
Na Zania Miraji
Chanzo BBC
Iraq imeomba rasmi usaidizi wa Marekani kushambulia kwa ndege wapiganaji wa
kiislamu walioteka miji kadhaa nchini humo wiki hii.
Katika
taarifa yake kwa taifa, waziri mkuu Nouri AL Maliki ametoa wito kwa raia wa
Iraq kuungana dhidi ya wanamgambo.
Vikosi
vya jeshi vinajitahidi kuwakabili na kuwasukuma nje wanamgambo wa ISIS pamoja
na washirika wao wa Ki-sunni kutoka mikoa ya Diyala na Salahuddin baada ya
waasi hao kuteka mji wa Mosul wiki iliyopita.
Taarifa
kutoka katika ikulu ya White house zinasema kuwa Rais Obama amependekeza
kuongezwa juhudi nchini Iraq za kusaidia
majeshi ya serikali hiyo katika kukabiliana na wanamgambo wa ISIS ikiwemo
uwezekano wa kuongeza usaidizi wa kiusalama.
Na zania Miraji Chanzo
BBC
Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za kisheria kupinga amri ya
kutumikia kifungo chake cha jela nchini Uingereza.
Bwana
Taylor amekataa kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa haki
ya kufurahia maisha yake huku Mawakili wake wakisema kuwa kuzuiliwa kwake
nchini Uingereza kunakiuka haki za binadamu.
Mawakili
hao wamesema badala ya kutumikia kifungo Uingereza, aruhusiwe kutumikia kifungo
hicho nchini Rwanda, pamoja na wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama
maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.
Charles
Tayor anatumikia kifungo cha miaka hamsini jela kwa makosa ya ubakaji na
kutumia watoto kama wanajeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini
Sierra Leone.
Na Zania Miraji
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment