Vikundi shirikishi vya polisi jamii katika manispaa ya Dodoma vimeelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili a wakati wa kutoa
elimu ya ulinzi na usalama.
Akizungumzana kituo hiki mkaguzi
msaidizi wa jeshi la polisi Bw George
Andala amesema baadhi ya wazazi hawapo tayari kutoa michango kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo
.
Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki katika mafunzo hayo ya polisi jamii yaliyo fanyika katika shule ya Sekondari Hombolo wamesema wamejifunza mambo mengi
ikiwemo kujenga ushirikiano pamoja na
kuwa na umoja .
Nae Diwani wa kata ya hombolo bw
musa kawea amewataka wanafunzi kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwa mfano
kwa wanafunzi wengine .
Na Nazael Mkude
chanzo Dodoma fm
Serikali
Kupitia wizara ya nishati na madini imesema kuwa imepeleka zaidi ya wanafunzi
mia mbili nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ya Gesi Asilia.
Akijibu Swali la Mbunge wa lindi Salimu Baruani, Naibu waziri wa Nishati na Madini Mh.Charles Kitwanga amesema
kuwa mpango huo unawapeleka wanafunzi
nje ya nchi kwa ngazi ya stashada,na
Uzamili,ambao wote watakuwa
wanatumikia sekta hiyo hapa nchini
Aidha waziri kitwanga amesema kuwa wizara
ya nishati na madini imekua ikitoa kipaumbele kwa kuwafadhili wanafunzi
wa maeneo yenye nishati asilia kama mtwara na lindi kupata mafunzo juu
ya rasilimali hizo.
Kuhusu tatizo la wanafunzi wengi
kutokidhi viwango vya kimataifa mara baada ya kihitimu masomo yao waziri
kitwanga amesema kuwa mpaka sasa wameboresha na wanaendelea kuboresha mitaala
ya vyuo vya ufundi stadi ili kukidhi hitaji hilo.
Na Stanley Msigwa chanzo
Bunge
Serikali imeombwa
kuwekeza fedha nyingi kwenye sekta amabazo zinaweza kuliingizia taifa kipato
kikubwa.
Ushauri huo umetolewa bungeni na mbunge wa Kigoma kusini
Bwana Moses Machali alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya serikali kwa
mwaka wa fedha 2014/15 unaoendelea mkoani hapa.
Aidha Bwana Machali ameongeza kuwa kwa kuendeleza utaratibu
wa kupeleka fedha nyingi kwenye sekta za kihuduma nchi haiwezi kuimarika
kiuchumi.
Kwa upande wake bwana Festus Limbu amesema serikali haiwezi
kutekeleza miradi mikubwa kwa kutegemea mapato yasiyo kuwa ya serikali na
mikopo peke yake ili ipate maendeleo.
KITAIFA
Wakulima wameaswa kuondokana na
kilimo cha mazoea, badala yake watumie kanuni bora za kilimo ili waweze
kuongeza kiwango cha uzalishaji na kipato katika familia zao.
Akizungumza katika maadhimisho
ya Siku ya Wakulima ya uboreshaji wa
mimea jamii ya mikunde yaliyofanyika
Kata ya Singe wilayani Babati Mtafiti Mkuu wa Kituo cha Utafiti Seliani Arusha
(Sari), Steven Lyimo amesema ni
vema wakulima wakaachana na kilimo cha
mazoea ili waongeze uzalishaji.
Aidha amesema kutokana na mabadiliko ya tabianchi, wakulima wanalazimika
kutumia mbegu za muda mfupi na kati ili waweze kupata wigo mpana wa uchaguzi wa
mbegu anapotaka kwenda shambani.
Sanjali na hayo
aliwambia wakulima ni vema kupanda aina za mbegu kulingana na kiasi cha mvua
mfano mwaka ambao hakuna
mvua unapanda mbegu ya muda mfupi na
mwaka ambao kuna mvua kiasi unapanda mbegu ya muda wa kati na mwaka
ambao kuna mvua ya kutosha unapanda ya muda ya muda mrefu.
Na mariamu kasawa chanzo
Mwananchi
KIMATAIFA
Wachunguzi
kutoka jumuiya ya mataifa ya eneo la maziwa makuu wamechapisha ripoti kuhusu
mapigano ya hivi karibuni yaliyotokea katika eneo la mpaka wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.
Ripoti hiyo inasema kuwa mapigano hayo
yalitokana na mzozo wa ardhi kati ya mataifa hayo mawili
katika maeneo ya milima miwili.
Wanachama wa tume hiyo walitembelea pande zote mbili
za mpaka na kuthibitisha kuwa Rwanda ilikuwa ya kwanza kulalamika kufuatia
habari za wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuvuka na kuingia
nchini Rwanda kwa lengo la kutaka kuiba ngombe.
Ripoti hiyo inasema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo kwa upande wake inasema kuwa Rwanda mara kwa mara haiheshimu mpaka ulio
kati ya mataifa hayo mawili na wanajeshi wake huvuka mara kwa mara na kuingia
katika taifa hilo.
Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mapigano ya hivi
majuzi yanatokana na kutokuwepo mpaka kamili kati ya mataifa hayo mawili.
Na mariamu kasawa chanzo
BBC
Watu ishirini wameuawa katika shambulio lililotokea
katika kijiji kimoja kilichopo kaskazini Mashariki mwa
Kenya.
Mwandishi wa BBC anasema watu wenye silaha walivamia
kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili ambapo
mapigano hayo yalizuka kutoka na mgogoro wa mpaka baina ya koo mbili za Degodia na Gare.
Pamoja na kwamba kuliwahi kutokea mapigano mengine
hapo awali lakini hayajawahi kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja kama
ilivyotokea siku ya jumapili.
Mauaji haya yanakuja wiki moja baada ya watu wapatao
60 kuuwawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la Mpeketoni katika
pwani ya Kenya lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al Shabaab
Na mariamu kasawa chanzo
BBC
Mahakama
nchini Misri imewahukumu jela miaka saba wandishi watatu wa habari wa shirika
la habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.
Waandishi
hao walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na
kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.
Mmoja wa
wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandihi
wa habari wa BBC .
Na mariamu kasawa chanzo
BBC
0 comments:
Post a Comment