Na Mariam Kasawa
Maafisa wa wizara ya ulinzi nchini Ukraine wamesema kuwa waasi wanaotaka
kujitenga ambao wanaiunga mkono Urusi wamelipua ndege iliyokuwa imewabeba
wanajeshi wa serikali na kuwauwa watu tisa.
Shambulio hilo lilifanywa karibu na mji wa Sloviansk
unaodhibitiwa na waasi mashariki mwa taifa hilo ambapo kwa mujibu wa maafisa wa
Ukrain wamesema helkopta hiyo ilipigwa risasi nje ya makao makuu ya Sloviansk .
Kutunguliwa kwa
helikopta hiyo kumetokea muda mfupi baada ya Serikali na upande wa kundi
linalotaka kujitenga kutoka kwa Ukraine kutangaza usitishaji wa mapigano.
Mnamo Jumanne Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alitoa wito
kwa Wabunge kubadilisha upigaji kura walioufanya mwezi Machi ambao
uliomruhusu yeye kuwa na mamlaka
ya kuingilia kijeshi maswala ya Ukraine.
Na Mariam Kasawa
Maelfu ya wafanyakazi wa migodi ya dhahabu nyeupe nchini
Afrika kusini wamerudi kazini kufuatia makubaliano ya malipo yao ya miaka
mitatu ya kumaliza mgomo ambao umedumu kwa muda wa miezi mitano.
Baada ya kutokuwa kazini kwa muda mrefu wafanyikazi hao
watapewa mafunzo na kufanyiwa ukagauzi wa kiafya nahuenda ikachukua miezi kadha
kabla ya shughhuli kwenye migodi kurejelea hali ya kawaida.
Mgomo huo unakisiwa kugharimu makampuni hasara ya dola
bilioni mbili na kusababasha kudorora kwa uchumi wa afrika kusini.
Wafanyakazi hao hawakupata mshahara waliotarajia wa Rand
za Afrika Kusini 12,500 (zaidi ya Dola 1,000) lakini walikubali mkataba wa
miaka mitatu ambapo wataendelea kuongezwa mshahara, penisheni, malipo ya nyumba
na bima ya Afya.
0 comments:
Post a Comment