KITAIFA
Na lucas godwini
Serikali
kupitia wizara ya Viwanda imesema hairuhusu kutumia kuni na magogo kwa ajili ya
uzalishaji viwandani hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara
Bi Janneth Mbene alipokuwa akijibu swali
la mbunge wa viti maalumu Bi Magdalena Sakaya lililohoji ni viwanda vingapi
vinatumia kuni na magogo katika uzalishaji na viwanda vingapi vinavyoruhusiwa
kutumia nishati hiyo
Aidha Waziri Mbene ameongeza kuwa serikali imekuwa
inachukua hatua kali kwa viwanda vyote vinavyokiuka sheria na kanuni ya ukataji
wa miti.
Sanjari na hayo Bi. Mbene ametanabaisha kuwa sheria ya
misitu ya mwaka 2002 inazuia uvunaji wa miti usio endelevu hivyo viwanda
vinavyokiuka masharti ya serikali vitaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Na happness
chesko
Wakazi
wa mtaa wa swaswa Manispaa ya
Dodoma wametakiwa kufahamu matumizi ya mabwawa ya maji taka katika
kilimo cha umwagiliaji.
Wakizungu na Dodoma fm wakulima wanaolima mbogamboga katika mabwawa
hayo ya maji taka wamesema maji hayo yanawasaidia katika kilimo cha umwagiliaji kwani wamekuwa wakilima mbogamboga kwaajili
ya biashara.
Nae Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa swaswa Bw. Chares Nyumba amesema hakuna elimu yoyote
waliyopewa wakulima hao juu ya matumizi ya maji hayo hivyo anawaomba wakulima wawe na subira ili
waombe mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira waje kutoa elimu.
Akizungumzia suala hilo Mkuu wa mawasiliano wa
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bw. Sebastiani Warioba
amesema ni vema wakulima hao wakatambua
kuwa maji wanayotakiwa kuyatumia ni ya mabwawa ya mwisho kwani ndiyo yanayo
ruhusiwa baada ya kujitibu.
Kilimo cha umwagiliaji kinaweza kikaleta tija katika
mkoa wa Dodoma kama kitazingatiwa kwa ufasaha hivyo ni vema serikali ikaboresha
miundo mbinu ili wakulima waweze kunufaika na kilimo hiki.
Na Stanle Msigwa
Wazazi
na walezi katika manispaa ya Dodoma wamelezea changamoto
zinazopelekekea ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumza na Dodoma fm mlezi wa kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu
(KISEDETI) bw. Kiweku Mpoto amesema wazazi hawatoi ushrikiano hasa kwa
watoto katika malezi hivyo kusababisha tatizo hilo.
Nae bi. Mwashi Katema
ambaye ni mlezi amesema watoto wanapata tabu kutokana na hali ngumu ya
maisha na sababu mbali mbali zinazo
tokea katika jamii zinapelekea hali hiyo kutokea .
Kwa upande wao watoto wanaoishi katika mazingira magumu
wameiomba serikali iwasaidie watoto waliopo
mitaani kurudi nyumbani.
Na Livingstone mwangingo
Wakazi
wa manispaa ya Dodoma wamelalamikia upandaji wa nauli kiholela katika mabasi
yaendayo mikoani hususani kipindi cha likizo.
Wakizungumza
na Dodoma fm wakazi hao wamesema kupanda
kwa nauli kunachangiwa na mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi kavu
(SUMATRA) kwani imekuwa haitoi taarifa
kwa wananchi.
Nae Bw, Dismon Kiwaye amesema kuwa mamlaka husika inashindwa kusimamia kupanda
kwa nauli kiholela kutokana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kumiliki
mabasi .
Akijibu
malalamiko hayo Kaimu Afisa
Mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi kavu
Bw. Ezekiel Emmanuel amesema wametoa nauli
elekezi ambazo wamiliki wa mabasi wanatakiwa kuzingatia na si kupandisha
nauli kiholela.
0 comments:
Post a Comment