Na Stanley Msigwa
Kufuatia kauli ya
shirika la maji safi na maji taka pamoja
na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma DUWASA
kuwataka wakulima wa mboga katika bwawa la Swaswa kata ya Ipagala katika
manispaa ya Dodoma kusitisha shughuli hiyo kutokana na usalama kiafya, wakulima
wa eneo hilo watoa maoni juu ya kauli hiyo.
Wakizungumza na kituo
hiki Baadhi yao wamedai kuwa maji taka
hayo ndio chanzo Kinachowapelekea wao kuendesha maisha ya kila siku na kudai
kuwa kama serikali haita watafutia bwawa jingine hawapo tayari kuacha kilimo hicho.
Nae mwenyekiti wa mtaa huo bwana Charlse Nyoma
amesema kuwa mtaa huo wenye jumla ya Wakazi
zaidi ya elfu Nne na Mia Saba na asilimia kubwa wanategemea kilimo cha
umwagiliaji kupitia bwawa hilo.
Aidha bwana nyoma
amesema kuwa serikali ina mipango mingi ambayo haitekelezeki na wakati huu wapo
kwenye mkakati wa kuzungumza na DUWASA
ili kujua jinsi gani ya kutatua tatizo hilo.
Kwa upande wake Bwa
Sebastiani Afisa habari wa DUWASA
amesema kuwa maji hayo si salama kwa matumizi kwani maji hayo yanatokana na
matumizi ya watu majumbani na Kutoa tamko la kuwa hayaruhusiwi katika kilimo
hicho.
0 comments:
Post a Comment