UKianza kutafakari kwa kina maelezo aliyoyatoa wiki hii Daktari Charles Masonde wa NECTA Utagundua Kuwa Wasomi Uchwara Tulio nao Wanatengezwa na Uroho wa Pesa na Sifa Kwa UMMA,
Mkururu wa Maelezo aliyotoa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr Masonde Utagundua Kuwa Matokeo ya mitihani Kila yanapotoka Shule za watu binafsi ama Asasi zisizo Za serikali ndo zinaongoza Kufaulisha.
Yaani Shule Bora zote ni Binafsi na Hata zile za UMMA za vipaji maalum Zimekachwa:Eboo!!!!!
wakati kila Idara/wizara ya serikali ikiwajibika kujinusuru Mikononi mwa mwenye rungu wasijekong'otwa ndipo uozo uliotukuka unaanza kupatikana kila kona.
Sasa leo Naamini(Binafsi) kwamba hizi shule Binafsi zipo kibiashara zaidi na kutengeneza wasomi Uchwara wa Kesho na sio Watalaamu ambao Akili za watanzania Zinategemea Watazalishwa katika Shule hizo.
Kama kweli Shule za watu binafsi zipo kwa ajili ya kutengeneza wasomi bora/wataamu bora pamoja na kuleta ushindani katika elimu ya tanzania kweli utumbo uliotengeneza na shule hizi mashughuli hapa nchini ni Aibu Kubwa sana.
Inawezekana Vipi shule wanaosoma ni watoto wa Vigogo ama watoto wa Mabwenyenye na Walimu wanalipwa vizuri,Vitendea kazi vipo, miundombinu yote ipo na watoto wanazingatia vigezo vya ufaulu wakati wa kujiunga inakuwaje walimu wafanye mitihani badala ya wanafunzi?.
01: SHULE YA MSINGI TUMAINI-SENGEREMA-MWANZA.
Mmiliki wa shule Hiyo aliyetajwa kwa majina ya JAPHARY MAHUNDE.huyu alifanya mtihani wa taifa na walimu wakena kisha kuwapa majibu watahiniwa na wakayaandika ndani ya sketi zao na kaptura zao,na mwisho wa siku darasa zima aliekosa swali la kwanza wote hivyo hivyo.
Na hapa Wizi Huu wa kuziba upeo kwa vijana wetu alishirikiana msimamizi wake Ndugu-Alex casiano Singoye,
02:SHULE YA MSINGI LITLE FLOWER-SERENGETI-MARA
shule hii nayo Mwalimu Mkuu wake Bi CESILIA NYAMOLONGA Kaandaa Majibu kawalaghai wasimamizi Ndugu HAROUN MUWI na Bi.JENIPHER SAIMON Nao Wakalidhia na wakawa wanagawa wenyewe majibu kwa watahiniwa wale.
03:SHULE YA MSINGI MIHAMA KUMI-SKONGE-TABORA.
Hapa ndo Pumba kabisa Walimu wa shule Hii wakajifanya nao ni watoto wa darasa la saba na wakaanza kujichukulia zile fomu za OMR Za kujibia Mtihani.Walichokifanya ni kwamba wakati wanafunzi wakiwa darasani wanaendelea na mtihani Huko chobingo nako Timu ya walimu inaendela na Kufanya mitihani na ikifika mda Mwalimu anaingia darasani anawagawia wanafunzi yale majibu waliyojabu wao na karatasi ya mwanafunzi inaondolewa,
Hapa wasimamizi nao walikluwa wanajua.
KUMBUKA HUU NI MFUMO MPYA WA KUJIBU MTIHANI AMBAO SERIKALI ILIONA NI MUAROBAINI WA WIZI WA MITIHANI NA KUVUJISHWA.
Uharamu Huu ulifanywa na Mwal.Kaombwe Samweli,Leonard Maleta Endrew, Michael Gilbert,na John Puna,chini ya msimamizi wao Fatuma Suleiman.
04:SHULE YA MSINGI KASHI-BABATI-MANYARA.
Huku nako walimficha Mwalimu ASHA YUSUPH MOSHA Chooni Mda Wa mtihani Ili awe anawapa wanafunzi majibu mara baada ya wao kuomba ruhusa ya kupiga simu Fupi au ndefu huku mwnafunzi huyo akitakiwa kuenda na karatasi la maswali na mwalimu ayajibu ili arudi akasambaze na kwa wenziwe.
05:SHULE YA ST.GERTUDE-MADABA-RUVUMA.
Hii shule ilijitengenezea Mfumo BRN kimatokeo kwa masomo yote,Mkuu wa shule hii Aliandaa Timu ya walimu wakaenda kukaa Bwenini na Nyumba moja ya mwalimu ya karibu ili wanafunzi wakitoka darasani mara baada ya kuomba ruhusa waende wakawape maswali na wao wafanye kisha wanafunzi wakagawane huko darasani pasi mlinzi kujua!!!!!!
Na mkakati wao Ulikuwa ili wapate mda wa kudokolezana ni kumsumbua msimamizi kila wakati ili awe bize.
kamati ufundi katika Wizi huu bila huruma uliongozwa na MwalimuFridolina Yohaness Mwalongo,Michael Mwafongo,Leonard Haule,Samsoni Mwaijibe,January Hongoli,Alkano Kisakari,Tna heodata Hyena.
HIZI NI BAADHI TU MABENCHI YA UFUNDI YALITELEZA YAKADAKWA JE VIPI AMBAO HAWAJADAKWA????
NA TUNAJIHAKIKISHIA VIPI KUWA SHULE ZILIZO KWENYE 10 BORA SI MOJA NA HIZI??
NA HII NI TAMAA YA NINI??
TUJITATHIMINI NA ELIMU YETU ILIPO SIPO!!
NA SHULE ZILIZOTENDA HIVYO NYINGIZE NI BINAFSI HII NINI TAFSIRI KWA UMMA WA WATZ????
Msigwa Stanley-Moshi.0658 001 999.
HIYO VIDEO NI DR CHARLES MASONDE-KATIBU MTENDAJI NACTE AKIELEZEA MADUDU HAYO
0 comments:
Post a Comment