Na-MwandishiWetu,Singida.
MDAI
katika Kesi ya madai ya talaka Magreth Mwangu dhidi yaMkurugenzi wa Shule ya St. Mathew, Thadei
Mtembei amehoji uhalali wamahakama kufikia kukagua mali zake siku ya
Jumamosi bila kupitiamahakama yoyote hapa Singida.Kesi hiyo ambayo inasikilizwa mahakama ya Mwanzo
Kizuiani MbagalaJijini Dar es Salaam, juzi (Jumamosi)
ililazimika kuhamia mkoaniSingida baada ya mdaiwa (Thadei Mtembei) kuitaka
mahakama kuhamiamkoani Singida kwa gharama zake ili kuhakiki
nyumba ambazo alidaialimjengea Mwangu.Mtembei katika hoja yake ya kuitaka mahakama
kuhamia Singida alisemayuko tayari kulipa gharama zote ikiwemo nauli na
posho.Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Rajab Tamaambele,
na wakili wa Mtembeiambaye ni mtoto wa mke mkubwa wa Mtembei (Peter
Mtembei), karani nakesi na mtumishi wa mahakama ni miongoni mwa
watu waliofika kwa ajiliya ukaguzi na uhakiki wa nyumba hizo.Hata hivyo hakukuwepo na wazee wa baraza jmbo
ambalo mwangu pia alililalamikia.Mwangu alidai kuwa licha ya kuwa hafahamu sheria
kutokana na kutokuwana elimu hata ya Sekondari lakini kitendo ha
mahakama kufika Jumamosikwa ajili ya kufanya uhakiki na ukaguzi haioni
kama ni ha haki na piakulikuwa hakuna afisa ustawi wa jamii.Alidai hakimu kuongozana na wakili wa kesi
hiyo na kuwa pamoja mudawote haoni kama atatendewa haki katika shauri
hilo.“Mimi nahoji ushirikiano huu kama hautanitendea
haki kwani watuwametoka pamoja Dar es Salaam wameongozana
kwenye magari binafsinafika eneo la tukio nakuta msafara wa hakimu, wakili
wa mdaiwa,mwenyekiti wa kitongoji ukiwa umeshafika mbele
ya nyumba ambayowalitaka kuanza kuihakiki” alidai.Alidai hata mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba,
Mahamoud alisema hajapewataarifa yoyote ya maandishi kwani alishtukizwa
na kupelekwa kwenyenyumba hiyo ambayo alisema hafahamu kama ni ya
Mwangu.Pia alihoji uhalali wa mtoto wa Mtembei ambaye
ni wakili kusimamiashauri hilo katika mahakama ya Mwanzo huku mara
kadhaa akimtoleamaneno ya kashfa kama ni mfunga vidonda tu
hawezi kujenga nyumba.Mwangu alisema alishawahi kuiambia mahakama kuwa
nyumba zake zaSingida alizijenga na aliamua kuziuza kwa ajili
ya elimu ya watotowake ambao walitelekezwa na baba yao lakini cha
kushangaza mahakamakwa amri ya Mtembei ikataka kufika Singida
kuhakiki nyumba zake.Hata hivyo mahakama ilikagua nyumba tatu ambapo
moja ilikuwaimeshauzwa kwa Sh. Milioni 15 na nyingine
iliuzwa ikiwa katika hatuaya msingi.Baada ya kumalizika kwa uhakiki huo hakimu
Tamaambele alimtaka Mwangukuhakikisha anawasilisha mahakamani nyaraka zote
za nyumba nakuwapeleka watoto mahakamani kabla ya kesi hiyo
kutolewa hukumu Agosti25, mwaka huuMwisho
0 comments:
Post a Comment