Ukarabati wa barabara ya mto kasimba umeenza kutokana na ujio wa mwenge
wa uhuru july 20 mwaka huu.
Mpanda radio fm imzungumza na mwenyekiti wa mtaa wa msasani bw.jonald
makoli ambapo amethibitisha kuwa
halmashauri imesha mkabidhi mkandarasi ambaye ameshaanza kuweka kifusi kwa
ajili ya kuweka sawa barabara hiyo itakayopitiwa na mwenge wa uhuru mkoani
hapa.
Bw.makoli ameongeza kuwa bajeti ya mwenge ndio inayotumika kutengeneza
barabara hiyo kutokana na wao kutotengewa bajeti yake.
Sanjari na hayo amewataka wananchi kutokuwa na hofu kufatia kuvunjwa
kwa mabaraza ya madiwani na kusitishwa
kwa shughuli za wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwani shughuli zote za maendeleo zitaenda
ipasavyo
Utengenezaji wa barabara ya
inayounganisha mpanda hoteli,msasani,na majengo kupitia mto kasimba
umekuja mara baada ya mwenge wa uhuru kutakiwa kukagua na kuzindua ujensi wa
maabara katika shule ya sekondari kashaulili ambapo barabara hiyo ndiyo
itakayotumika.
0 comments:
Post a Comment