MKUU wa Mkoa wa Katavi
Dk. Ibrahim Msengi amesisitiza kuwepo kwa amani, upendo na ushirikiano kwani
itakuwa ni fursa nzuri kwa watu kufanya shughuli za maendeleo.
Dk. Msengi ametoa
kauli hiyo jana katika hafla fupi ya kufuturisha iliyofanyika Ikulu ndogo mjini
Mpanda.
Amewataka wakazi wa
mkoa wa Katavi kuondoa tofauti za itikadi za kidini na kisiasa na badala yake
wadumishe amani na kuepukana na vitendo viovu, kwani Watanzania wote ni wamoja
na wanashirikiana katika kila.
Amewataka wakazi wa
mkoa wa Katavi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapoona kuna dalili za
uvunjifu wa amani ili hatua za haraka zichukuliwe.
Hafla hiyo fupi ya
futari, ilihudhuriwa na viongozi wa dini wakiongozwa na askofu wa kanisa la New
harvest Afrika mashariki na kati Askofu Laban Ndimubenya, viongozi wa serikali,
waumini wa dini mbali mbali na waandishi wa habari.
TAZAMA PICHA HAPO CHINI>>
Picha zote na Msigwa Stanley
 |
WA PILI KUSHOTO NI MKUU WA MKOA WA KATAVI DR.IBRAHIM MSENGI |
 |
SHEIKH MASHAKA AKIONGOZA SWALA |
 |
MKUU WA MKOA WA KATAVI (KATIKATI)AKIPATA FUTARI NA VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU-MKOA WA KATAVI |
 |
KATIKATI NI ASKOFU LABAN NDIMUBENYA WA NEW HARVEST CHURCH |
 |
RPC.MKOA WA KATAVI DHAHIRI KIDAVASHARI AKIFUTURU. |
 |
WAWAKILISHI KUTOKA DINI YA KIKIRSTO,WA KWANZA KUSHOTO NI FATHER WA JIMBO KUU LA MPANDA ROMAN CATHOLIKI NACLETUS BAFUMKEKO |
 |
MKUU WA MKOA AKISIKILIZA SHUKRANI KUTOKA KWA MWAKILISHI WA SHEIK MKUU KATAVI.(ALIESIMAMA) |
 |
MIONGONI MWA WAUMINI WALIO HUDHURIA HAFLA HIYO KATIKA VIUNGA VYA IKULU NDOGO MPANDA MJINI. |
0 comments:
Post a Comment