Na Mwandishi Wetu
MDAI katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali Magreth Mwangumkazi wa Mkoani Singida dhidi ya Mkurugenzi wa Shule za sekondari zaSt.Mathew na St Marks Thadei Mtembei amelalamikia kitendo cha Benki yaCRDB kutoa taarifa zake za benki bila idhini yake wala ya mahakama.Pia ameilalamikia mahakama ya Mwanzo Kizuiani inayosikiliza kesi hiyokwa kutumia Wakili wa kujitegemea licha ya kuwa mawakili hawaruhusiwikatika mahakama ya Mwanzo.Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Rajab Tamaambele.Wakili huyo amekuwa akimwakilisha mdaiwa ambaye amekuwa hafikimahakamani tangu kesi hiyo ifunguliwe kwa kile kilichoelezwa wamepatakibali kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kinachoruhusu kesi hiyokusikilizwa na wakili bila mdaiwa kuwepo.Kwa mujibu wa Mwangu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapomdaiwa amekuwa hafiki mahakamani na badala yake amekuwa akiwakilishwana mtoto wake,Peter Mtembei ambaye ni Wakili hali iliyofanya kesi hiyompaka inaisha na kufungwa ushahidi mdaiwa akiwa hajasikiliza shahidihata mmoja.Hata hivyo Mmiliki huyo wa St, Mathew juzi alifika mahakamani kufuatiaamri ya mahakama kufuatia malalamiko ya mdai aliyokuwa akitoamahakamani kutokana na Mtembei kushindwa kufika kwenye kesi hiyo tanguilipofunguliwa na iliyomtaka afike mwenyewe mahakamani hapo na endapoasingefika mahakama ingehamia nyumbani kwake.Akitoa ushahidi wake, Mtembei alisema alifahamiana na Mwangu wakatiakiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa nayewatoto watatu.
Alisema mama huyo hana hadhi ya kuwa mke wake kwani ameishia darasa lasaba elimu ambayo ni ya chini sana.“Huyu alikuwa ni mfanya usafi tu ni nesi msaidizi kazi yake ilikuwa nikufanya usafi na hata kufunga vidonda tu” alisemaAlisema duka hilo la dawa lilifungwa baada ya kuonekana aliyekuwaanalihudumia hana elimu.Mtembei alisema mdai hana uhusiano na mali alizonazo kwani yeye anamke wake wa ndoa na huyo alikuwa ni mwanamke tu aliyezaa naye.“Huyu ni mwanamke tu niliyezaa naye hana haki kwenye mali zangu” alisemaAlipohojiwa na mahakama kama alifunga ndoa na mdai alisema kuwahajawahi kufunga naye ndoa licha ya kutoa mahari ya ng’ombe watano.“Nilimpelekea baba yake vindama vitano tu kama zawadi” alisemaAlisema hajawahi kufunga ndoa ya kimila na mdai kama inavyodaiwa namdai hana haki yoyote katika mali zake.Kwa upande mwingine mdai alihoji sababu za mdaiwa kwenda Benki ya CRDBna kutoa taarifa za fedha za akaunti yake bila kuwa na amriiliyotolewa na mahakama.“Mdai kwa kutumia nafasi nzuri ya kifedha aliyokuwa nayo amewezakwenda benki ya CRDB na kupewa taarifa za fedha kwenye akaunti yangubila ruhusa yangu au ruhusa ya mahakama jambo ambalo limeniathirikisaikolojia’ alisemaHata hivyo hakimuTamaambele alisema hafahamu ni wapi mdaiwa alitoataarifa hiyo lakini mahakama inaipokea kuwa sehemu ya ushahidi.Kesi hiyo imepangwa kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka huu.Katika kesi hiyo mdai anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa kupatakala,kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
CHANZO CHA STORY HII..http://ngelangelanews.blogspot.com/2015/07/hii-ni-story-ya-kweli-na-inasikitisha.html
0 comments:
Post a Comment