Basi Lililobeba Mashabiki Wa Yanga Wanaokwenda Kuishangilia Timu Yao
Keshokutwa, Tayari Limewasili Nchini Zimbabwe.
Basi Hilo Aina Ya Toyota Costa ‘Mayai’ Limetua Kwenye Mpaka Wa Zimbabwe
Leo Asubuhi Na Walitarajia Kukanyaga Ardhi Ya Nchi Hiyo Leo.
Hata Hivyo, Bado Watakuwa Na Safari Ndefu Na Wanatarajiwa Kuwasili
Harare Leo Mchana Kabla Ya Kuanza Safari Nyingine Ya Kwenda Bulawayo Ambako Yanga
Itapambana Na FC Platinum Katika Mchezo Wa Pili Wa Kombe La Shirikisho.
Mmoja Wa Mashabiki Walio Katika Basi Hilo Amesema Wamekuwa
Wakiendelea Vizuri. Msafara Wa Basi Hilo, Pia Yumo Mzee Wa Yanga, Ibrahim
Akilimali Ambaye Ameungana Na Vijana Kwenda Kuwapa Nguvu Yanga.
Rais Wa Shirikisho La Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi Amewatakia Kila La Kheri Wawakilishi Pekee Wa Tanzania
Kwenye Kombe La Shirikisho Barani Afrika (CC) Young Africans, Katika Mchezo Wa
Marudiano Dhidi Ya FC Platinum Ya Zimbabwe Utakochezwa Siku Ya Jumamosi Kwenye
Uwanja Mandava Uliopo Gweru Bulawayo.
Malinzi Amesema Young
Africans Hawapaswi Kubweteka Na Ushindi Walioupata Awali Wa Mabao 5-1, Kikubwa
Wanapaswa Kwenda Kupambana Kusaka Ushindi Ugenini Ili Kuweza Kufuzu Kwa Hatua
Inayofuata Ya Timu 16.
Endapo Young Africans Itafanikiwa
Kuwatoa FC Platinum Itaingia Katika Hatua Ya 16 Bora Na Itakutana Na Mshindi
Kati Ya Timu Za Benifica De Luanda Ya Angola Au Etoile Du Saleh Ya Tunisia.
0 comments:
Post a Comment