 |
kamanda wa pilisi mkoa wa katavi dhahiri Kidavashari.picha na maktaba |
Na Agnes Mnubi_katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewataka wananchi kusherekea sikukuu ya pasaka kwa amani na utulivu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Dhahiri Kidavashari wakati akizungumza na Mpanda fm Ofisini Kwake.
Pia Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema katika kuimarisha ulinzi na kuwashughulikia ipasavyo watu ambao watajihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kusherekea sikukuu ya pasaka.
Aidha ametoa pongezi kwa wananchi kwa ushirikiano wao juu ya kutoa taarifa za vitendo vya uharifu, na kuwataka kuzidi kutoa taarifa hizo wakati vitendo vya uvunjivu wa amani vinapotokea.
0 comments:
Post a Comment