Na Martha magawa ...Dodoma
Wakati kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zinaelekea ukingoni Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa (TAKUKURU) Imewataka wananchi kutojihusisha na masuala mazima ya kupokea rushwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bi. Emma Kuhanga alipotembelewa na Dodoma fm ofisini kwa lengo la kutaka kufahamu Taasisi yake imejipangaje kudhibiti vitendo vya kutoa au kupokea rushwa msimu huu wa uchaguzi kama anavyobainisha.
Aidha Bi .Kuhanga amebainisha adhabu zitakazo tolewa kwa mtuhumiwa ataebainika kupokea au kutoa rushwa ambapo ni pamoja na kupoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Sanjari na hayo amewataka wananchi kupingana na rushwa kwa kutopokea pamoja na kutoa taarifa mara tu wanapoona tabia ya rushwa inatendeka .
Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika nchi nzima Desemba 14 mwaka huu hivyo basi TAKUKURU nao hawapo nyuma kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haki na usalama.
0 comments:
Post a Comment