Na Andrew Chaopa
Madereva bodaboda Mkoani Dodoma wametakiwa kuwa na utaratibu wa
kupiga dawa mara kwa mara kofia
zinazovaliwa na watumiaji wa usafiri huo
ili kupunguza maambukizi ya magonjwa.
Wito huo umetolewa na Mganga
Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Mkoani Dodoma Dr.Nasoro Mzee alipokuwa akizungumza na Uhakika Info ambapo amewataka
madereva bodaboda wote kuzifanyia usafi kofia zao ili kuwakinga
watu na maambukizi ya magonjwa ya ngozi.
Aidha Dr.Mzee amewashauri abiria wanaotumia
usafiri huo kuvaa kofia ngumu
ili kupunguza athari zinazoweza
kutokea pindi inapotokea ajali.
Kwa upande wao madereva boda
boda Manispaa ya Dodoma wamepokea kwa
shingo upande kauli hiyo ambapo wamesema
ni zoezi gumu kwa upande wao hivyo kuitaka serikali kuliangalia suala hili la
kuvaa kofia katika maeneo ya karibu
0 comments:
Post a Comment