Na Prosper Mfugale-njombe.
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa njombe kibena inakabiliwa na uhaba wa kompyuta kwaajili ya kusaidia kuharakisha ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kielekroniki pamoja na kutunza taarifa ambapo kwa sasa kuna kompyuta 8 tu kati ya kompyuta 48 zinazohitajika.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo winfridi kiambile amesema kuwa mara baada ya kufungwa kwa mifumo ya kisasa ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi laki mbili mpaka milioni mbili kwa siku huku mganga mkuu wa mkoa dr bumi mwamasage akiwataka wadau mkoani njombe kujitolea kusaidia changamoto zilizopo hospitalini hapo.
Kwa kutambua changamoto hizo mfuko wa bima ya afya wa taifa NHIF Umechangia compyuta mbili ambazo zitatatumika Kutunzia taarifa.
0 comments:
Post a Comment