Tanzania Anthem

Friday, 14 October 2016

NEWS:MJUE ALIYE TOA WAZO LA KUHAMIA DODOMA

Leo katika kumbukizi ya HAYATI Mwal.J.K.Nyerere ,Acha mimi nimuenzi kwa kukumbuka jitihada za serikali yake kutaka kuhamia Dodoma jambo ambalo limeanza kutekelezwa kwa miaka 40’s mbele.

Mnamo mwaka 1966 Mdogo wake na Mwalimu ,aliye julikana kama Joseph Nyerere alipeleka hoja binafsi bungeni akitaka Serikali ihamishie makao yake Dodoma,Hoja iliyopingwa vikali na wizara ya Fedha palepale na kuwa serikali haina pesa za kutosha kuhamia mjini Dodoma.
Tangu hiyo mwaka 1966 huyu ndiye akawa amepanda wazo hili la kuhamia Dodoma na ndani ya bunge haikupata nafasi ya kujadiliwa Tena,Isipokuwa Serikali ilianza kuupalilia hili wazo la Mh joseph Nyerere,Mdogo Mtu.

Mwaka 1972 chama cha Tanu kilianza kupendekeza jambo hilo kwa mlengo wa chama ya kuwa chama hicho pamoja na serikali kwa ujumla makao makuu yake yawe Dodoma.(DAR ES SALAAM TO DODOMA)

Na hiyo ni katika kikao kidogo cha Tanu Huko mkoani Mwanza,na ikaja kuwa na nguvu hoja hiyo kupitia Azimio la Arusha lililokuwa na Dhima ya Kupiga vita Umaskini,Huku wakijiaminisha kuwa Isitumike pesa ambayo ni silaha ya tajiri (kosa) bali pesa iwe ni matokeo ya maendeleo ; “Masikini hatakiwi kutumia Fedha kama Silaha yake”(MWl.Nyerere kupitia azimio la Arusha.) Na ikaipa nguvu Zaidi Tanu KuifUata Wizara ya Fedha na kuiambia Suala hilo.

Hii ni Kwa mjibu wa Mzee Pius Msekwa aliekuwa spika wa Bunge.

Mwaka mmoja mbele (1973) jumla ya matawi 1859 ya Tanu Kote Nchini wakati huo walipiga kura ya kuridhia Serikali kuhamia Dodoma,na Ilipofika mwezi August 1973 Tamko rasmi kitaifa kutoka Tanu likatolewa ili serikali ihamie kikamilifu kwa mda usio zidi miaka 10.

BAADA YA MIAKA KUMI SASA.

MWAKA 1983 MDA ULIOPANGWA UKAPITA NA SERIKALI HAIKUHAMIA DODOMA ILA CHAMA CHA TANU NDO KILIHAMIA DODOMA KWA NINI ILI HALI MWAL.NYERERE ALIUNDA MPAKA WIZARA YA KUPANGA NA KUENDELEZA MJI MKUU:-

MH Mstaafu kisiasa Pius Msekwa Ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa mamlaka ya ustawishaji makao makuu (CDA)baada ya kuundwa na Mwalimu.,Anasema Sababu zake.

01. Vita ya Idd Amin (Kagera War 1978-79).
Hapa inaelezwa kuwa na Rasilimali watu na vitu vyote vilielekezwa kupambana na nguli huyo ili ashindwe na kuacha kukusanya fedha za kuhamia Dodoma.

02. Kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977.

Na hapa vilevile ile miradi na huduma zote zilizokuwa zikitolewa na jumuiya hii zilisimama na ikabidi serikali wakati huo ianze kutafakari jinsi gani wataweza kuhudumia na pesa zetu wenyewe.

03.ongezeko la bei ya mafuta maradufu duniani ikilinganishwa na awali.

Kupanda kwa bei ya mafuta kunaelezwa kuwa kulipelekea fedha za kigeni na ndani pia zianze kushughulikia suala la mafuta na sio huduma kama ilivyotegemewa.na huku ukihusisha mpango wa kuhama pahala kuna hitaji hela kiasi kikubwa.

Inasemekana wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere Hayo ndo mambo makuu matatu yaliyo kuwa kizuizi kuhamia Dodoma,usiniulize vipi kuhusu utawala wa wengine.
Na mwaka 2016 mwezi July Rais Dr Magufuli Alisema.

“Nataka kuwathibitishia katika kipindi cha miaka 4 na miezi 4 iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa.

Na Sasa ofisi ya waziri mkuu imeshahamia Mjini Dodoma 
.
PUMZIKA MAHALA PEMA PEPONI MZEE WETU,MATARAJIO YAKO YAMEANZA KUTEKELEZWA NA RAIS MFUATA NYAYO ZAKO.
MSIGWA STANLEY-MOSHI
0658 001 999.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive