Tanzania Anthem

Tuesday, 28 July 2015

RIGANGA NA MCHUCHUMA KUAJIRI ZAIDI YA 33,000.

Na Prosper Mfugale_Njombe.
Idara ya Uhamiaji nchini imejipanga kukabiliana na wahamiaji kutoka nje ya nchi wanaokuja kufuata fursa za uwekeza katika migodi ya madini ya makaa ya mawe Nchuchuma na  Liganga wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Katika mkutano wa maofisa wa uhamiaji wa mikoa yote nchini unaofanyika kwa siku saba mkoani  Njombe, maofisa hao wameazimia  wahamiaji  wanaoingia nchini kufuata taratibu za uhamiaji.
Migodi ya chuma na makaa ya mawe inatarajiwa kuleta watu wapatao zaidi elfu sita kutoka nje ya nchi, huku ikitarajiwa kutoa ajira zipatazo 33,000 kwa watanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, amewataka maofisa hao kuitafakari dhana ya mipaka katika kipindi cha cha kuelekea mwanzo wa uchimbaji wa migodi hiyo kwa kuimarisha mipaka kabla wageni hawajajipenyeza kwa njia sizizo  rasmi 
Mwenyekiti wa maafisa uhamiaji hapa nchini ambaye pia ni naibu kamishna uhamiaji mkoa wa dareslamu bw john sumule amesema dhumuni la kikao kazi cha maafisa uhamiaji mkoani njombe ni pamoja na kutembelea eneo la uwekezaji wa madini ya liganga na mchuchuma
Naye naibu kamishna uhamiaji mkoa wa njombe Rose mhagama amesema kuwa amekwisha kuomba msaada wa kuongezewa watumishi wa idara hiyo makao makuu ili kukabiliana na uwekezaji mkubwa siku za usoni wilayani ludewa
Wakibainisha changamoto katika kutekeleza majukumu yao baadhi ya maofisa uhamiaji wamesema kuwa kuna uhaba mkubwa wa watumishi unaopelekea wimbi la wamiaji kuendelea kushamiri kama anavyoeleza kamishna msaidizi uhamiaji kituo cha sirali  mkoa wa mara estumire gasper urio na mkuu wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wa abeid amani karume zanziba fulgency mutarasha
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive