Na Lutakilwa Lutobeka_Mpanda
Wananchi
wanaofanya kazi katika ya kupepeta mchele katika kata ya Mpanda hoteil wilayani
Mpanda mkoani KATAVI wameitaka serikali kuwapatia mtaji ili waachane na kazi
hiyo kwani ni hatari kwa afya zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari wa Mpanda redio bi JUSTINA ANTONY LUSINGE ameesema kuwa serikali imekuwa
ikiwafukuza katika shimo hilo hali ya kwamba shimo hilo ndilo linalowawezesha
kujipati fedha za kujikimu ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto wao,kujipatia
chakula, mavazi na hata kujenga.
Kwa upande wake bi
MWASI ANDREA ameongeza kuwa wanalazimika kuingia katika shughuli hiyo
kutokana na kukabiliwa na majukumu mbalimbali hasa ya kielimu licha ya shughuli
hiyo kuwa na madhara makubwa kwa binadamu kutokana na vumbi la mapumba hayo.
Hata hivyo
bi Mwasi ameishauri serikali iwasaidie kwa hali na mali ili kuyanusuru maisha
ya wananchi ho ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahindi pamoja na misaada
mbalimbali ya kijamii ili waondokane nakazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment