Licha ya zoezi la kuwarudisha
wanafunzi watoro kwa mkoa wa katavi
kufanikiwa kuwarudisha wanafunzi 78 wa
Kidato cha kwanza Mpaka cha nne Katika
shule za Sekondari,Ikola,Ilandamilunda,Mpanda ndogo na Kabungu,bado ugumu wa
maisha umetajwa kuwa ndio chanzo cha utoro huo.
Wakizungumza na Uhakika Info baadhi
ya wakazi wa mpanda hoteli wamesema kuwa uzembe wa wazazi na na ugumu wa maisha
ndio chanzo cha wanafunzi wengi kukatiza
masomo.
.
Nao baadhi ya wanafunzi waliokatiza
masomo kwa kigezo cha kukosa mahitaji yashule wamesema kukosa kwa mahitaji mhimu
ya shule yanapelekea wao kuacha shule na kutafuta vibarua kwa ajili ya
kujikimu.
Sanjari na hayo wakazi hao wametoa
mapendekezo ya nini kifanyike kwa wazazi wazembe juu ya ufuatiliaji wa
maendeleo ya watoto.
Zoezi la kuwarudisha watoto watoro na walioacha masomo
ilianza rasmi tarehe 12 mwezi huu ikiwa ni amri halali kisheria iliyotolewa na
mkuu wa wilaya ya mpanda Bw.Pazza Mwamlima
0 comments:
Post a Comment